Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi
Mhe. Josephat Kandege amewataka wauzaji, waagizaji, wasambazaji na wadau wote
wa dawa pamoja na Vifaa Tiba Nchini kuchangamkia fursa inayotolewa na Serikali
ya kuwa Mshitiri mteule ‘Prime
Vendor’ kusaidia katika utoaji wa dawa katika Mikoa yote Tanzania.
Kandege ameyasema hayo wakati
akifungua kikao cha Wadau wa dawa ‘Vendors
Forum’ kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na wadau wa
Afya ‘HPSS’ chenye lengo la kuweka
uelewa wa pamoja kuhusu uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo wa Mshitiri.
Amesema “mfumo huu utatumika kupata
mahitaji ya bidhaa za Afya pale ambapo vituo vya kutolea huduma za Afya vya
Umma vitakosa au kupata kiwango pungufu toka Bohari Kuu ya Dawa na pia
utasaidia kupunguza kero za Afya ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa dawa kwenye
vituo vya kutolea huduma za Afya”.
Sasa basi ninyi kama wazabuni muhimu
katika sekta hii ya Afya wenye Uzalendo na nia njema na Nchi ya Tanzania
mnatakiwa kujitokeza katika mchakato wa kumpata Mshitiri (Prime Vendor) wa kila
Mkoa ambaye atakidhi vigezo kwa mujibu wa taratibu manunuzi alisema Mhe.
Kandege.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege(mbele) akifungua kikao cha wadau wa Afya ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika Ukumbi wa Dodoma Hotel.
Mkurugenzi wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Ntuli Kapologwe akitoa maelezo ya awali kabla hajamkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao cha wadau wa Afya Vendor Forum.
Mfamasia Mwandamizi toka Ofisi ya Rais Tamisemi Regina Richard akielezea malengo la kikao cha Wadau wa Dawa ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel mapema leo.
Wataalam toka Idara ya Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau wa Dawa wakiwa katika kikao maalum cha wadau wa dawa.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege(mbele katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu na wadau wa dawa.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...