Na WAMJW, Dar es Salaam
Serikali
kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
imenunua mashine za Mionzi (digital X-ray) zipatazo kumi zenye thamani
ya shilingi bilioni 1.74.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu wakati akipokea mashine hizo kwenye Bohari ya
Dawa(MSD) jijini hapa.
Waziri
Ummy amesema kuwa Serikaki inaendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha
huduma za afya nchini ikiwa ni lengo la kuhakikisha huduma za afya
zinawafikia watanzainia wote karibu na maeneo wanayoishi.
"Maendeleo
ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye
uwezo wa kuzalisha mali,hivyo tunaboresha na kuimarisha huduma za tiba
na uchunguzi wa magonjwa katika hospitali zetu kuwa na vifaa vya kisasa
zaidi na kuondokana na utaratibu wa kupeleka wagonjwa nje ya
nchi".Alisema,Waziri Ummy Mwalimu.
Alisema
mashine hizo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa 10 ambazo
X-ray za zamani zimekwisha muda wake na zimekua zikiharibika mara kwa
mara.Alizitaja hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi,Morogoro,Njombe,Ruvuma, Simiyu na Singida pamoja na hospitali za Wilaya ya Magu na Nzega.
Aidha,Waziri
Ummy alisema katika bajeti ya mwaka 2018/2019, Wizara yake imepanga
kununua mashine za mionzi nyingine zipatazo ishirini na nne(24) zenye
thamani ya shilingi bilioni 4.1 ambazo zitapelekwa kwenye hospitali za
rufaa za Mikoa na Wilaya ambazo hazina au zina X-ray za kizamani au
chakavu.
Akizungumza
kwa niaba ya Waganga Wakuu wa hospitali zinazopelekwa mashine
hizo,Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana Dkt.Mashack
Shimwela alisema ujio wa mashine hizo za kisasa zitasaidia kupunguza
gharama za uendeshaji wa uchunguzi za mionzi pia utunzaji wa mazingira
tofauti na aina zilizokuwa zikitumika mwanzo
Aidha,alisema
mashine hizo zina ubora wa picha pia ina mifumo ya Tehama ambayo ni
rahisi kusomwa hata nje ya hospitali husika endapo hakuna msoma picha .
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akionesha baadhi ya mashine za mionzi 10 zilizonunuliwa na Serikali
zenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 na kusambazwa kwenye Hospitali za
Rufaa za Mikoa,pichani kushoto ni Mwakilishi wa kampuni ya Phillips Bi.Monica Joseph
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipewa maelezo mafupi kutoka kwa Muwakilishi wa Kampuni ya Philips Bi. Monica Joseph mara baada ya kukabidhi baadhi ya mashine za mionzi 10 zilizonunuliwa na Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 1.74 na kusambazwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipewa maelezo mafupi kutoka kwa Muwakilishi wa Kampuni ya Philips Bi. Monica Joseph mara baada ya kukabidhi baadhi ya mashine za mionzi 10 zilizonunuliwa na Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 1.74 na kusambazwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa
Waziri
Ummy akiongea na vyombo vya habari wakati wa kupokea mashine hizo za
mionzi (digital X-ray) ambazo zitaboresha huduma za afya nchini hususani
za uchunguzi wa mionzi
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt.Mashack Shimwela akiongea
na waandishi wa habari baada ya kupokea mashine hizo Picha zote na
Wizara ya Afya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...