Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limeanza operesheni maalumu ya kukamata bodaboda zote zinazoingia katikati ya Jiji ambapo ndani ya saa 24 wamekamata pikipiki 104. Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa wakati anazungumza na waandishi wa habari kuhusu operesheni ambazo wanazifanya.
Amefafanua Polisi wameanza operesheni ya kukamata waendesha bodaboda ambao wanaingia katikati ya mji wakati wamezuiliwa kuingia huko.
Kamanda Mambosasa amesema baadhi ya bodaboda ambazo zimekamatwa zimetokana na makosa ya kutovaa kofia ngumu kwa wanaoendesha, kupitia njia tofauti na utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria na kupakia mishikaki.
Kamanda Mambosasa amesema baadhi ya bodaboda ambazo zimekamatwa zimetokana na makosa ya kutovaa kofia ngumu kwa wanaoendesha, kupitia njia tofauti na utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria na kupakia mishikaki.
"Ni marufuku bodaboda kuingia katikati ya Mji,hatuwezi kuacha hilo likaendelea kufanyika.Walishakatazwa kuingia katikati ya mji." Mbali ya kuwakamata wanaiongia mjini pia tunaendelea na operesheni ya kukamata bodaboda ambazo zinatumika kutenda matukio ya uhalifu.Pia tutakamata bodaboda ambazo wanaoziendesha wanashindwa kufuata sheria za usalama barabarani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...