Taasisi
ya Hassan Maajar Trust (HMT), imeendeleza dhamira yake ya kuboresha
mazingira ya shule za msingi nchini, ambapo imekabidhi jengo la vyoo
shule ya msingi Pugu Kajiungeni, wilaya ya Ilala, Dar es Salaam. Jengo
hilo lililogharimu jumla ya Shillingi milioni 65,000.00 lina vyumba 12
na sehemu maalumu kwa wavulana -urinals, ambapo vyumba 2 ni kwa ajili ya
ya watoto wenye ulemavu na chumba cha staha kimoja (Dignity Room) kwa
ajili ya wasichana wenye mahitaji ya staha.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Maajar, alikabidhi vyoo
hivyo kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bi. Rophina Aloyce Kawishe, katika
hafla fupi iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema,
ambaye alikuwa mgeni rasmi, walimu, wanafunzi, na wawakilishi kutoka
Shirika la Water Aid.
Akiongea
katika hafla hiyo, Balozi Maajar amesema “Hii ni mara ya kwanza kwa HMT
kujenga vyoo vya shule, na tumefurahia kukamilisha mradi huu wa kwanza.
Kwa kipindi kirefu nyuma, HMT ilikuwa inajulikana kwa kampeni yake
kubwa ya ‘Dawati Kwa Kila Mtoto’ ambayo imefanikiwa kwa kutoa madawati
10,000, na kunufaisha zaidi ya wanafunzi 30,000 katika mikoa 13 nchini.
Tuliona
vilevile vile kuna changamoto ya uhaba wa vyoo mashuleni. Imekuwa fursa
nyingine ya Taasisi ya HMT na wafadhili wake kuunga nguvu kwa pamoja
kwa kampeni mpya yenye kauli mbiu, Vyoo Bora Kila Shule. Aidha amesema,
kila safari ni hatua ya kwanza na kwa mradi huu ndiyo hatua ya kwanza
kwa HMT kutimiza lengo la kujenga vyoo shule za msingi zilizo na
mahitaji na hasa shule zilizo na idadi kubwa ya wanafunzi wenye
ulemavu.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Maajar akitoa hotuba wakati wa hafla ya uzunduzi wa miundo mbinu ya vyoo katika shule ya msingi ya Pugu Kajiungeni ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia mjema, Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, walimu, wanafunzi, Maofisa ma maofisa kutoka taasisi ya HMT
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema( katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Vyoo bora 12 na vyumba Viwili kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaa, Wengine kwenye picha ni mwenyekiti wa Hassan Maajar Trust (TMT) Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wapili kulia) Mkuu wa shule ya msingi Pugu Kajiungeni,Ropiana Alponce (Kushoto) pamoja na viongozi wengine, Msaada huo umejengwa na Taasisi ya Hassan Maajar Trust.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akihutubia wageni waalika katika hafla hiyo.
Wanafunzi wasichana wakipokea baadhi ya zawadi zilizotolewa na marafiki wa taasisi ya HMT wakati wa hafla hiyo.
Mgeni rasmi akikagua miundombinu ya choo cha kisasa kilichojengwa na HMT chini ya mpango wake wa Vyoo Bora kwa Kila shule.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...