MAKOSA
mbalimbali ambayo yanafanywa na wanaoendesha vyombo vya moto barabarani
yamesababisha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupata
zaidi ya Sh.Bilioni 2.74.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa
amesema hayo leo ambapo amefafanua jeshi hilo linaendelea na operesheni
ya kuwasaka madereva wa magari na watumiaji wa vyombo vya moto ambao
hawazingatii sheria ya usalama barabarani.
Amefafanua
katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata magari madogo,maroli,
pikipiki na daladala ambapo wahusika wametozwa faini ambapo zaidi ya
Sh.Bilioni 2.74 zimepatikana.
Pia
amesema kuwa ni vema madereva kuhakikisha wanafuata sheria za usalama
barabarani huku akionya tabia ya baadhi ya madereva wanaondesha magari
huku wakichati muda wote.
Amesema ni vema wakaacha tabia ya kuendelea kutumia simu kwani madhara yake ni makubwa na ni sawa na kukitafuta kifo.
Pia
Kamanda Mambosasa amewawataka watu ambao wametozwa faini za barabani
kulipa kwa wakati kwani kuna tabia ya kulimbikiza deni na wataendelea
kuwasaka wadaiwa wote na iwapo watashindwa gari litachukuliwa na kuwekwa
Polisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...