Na Vero Ignatus, Liwale - Lindi

Hatimaye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale umemalizika kwa huku mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Zuberi Kuchauka akiibuka mshindi wa kiti cha ubunge. Msimamizi uchaguzi Jimboni hapo Luiza Mlelwa amesema waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 55777 na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 40706 kura halali zilikuwa 40,301 kura zilizokataliwa ni 405 

Akimtangaza mshindi wa kiti cha ubunge (6:30usiku ) Jimbo la Liwale msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Zuberi ameshinda kwa kura 34, 582 sawa na asilimia 85.81.Mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge Zuberi Mchauka amesema ameyapokea matokeo kwa furaha na ameahidi kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Liwale kutatua changamoto mbalimbali zilizopo

Aidha Mchauka amesema kuwa changamoto nyingi zilizopo katika Jimbo la Liwaleni pamoja na miundombinu ya barabara, maji, Elimu, mawasiliano na Afya ambapo ameahidi wananchi kuwa atashughulikia changamoto hizo. 

Abdul Kombo Ngakolwa mgombea wa chama cha (AAFP) chama cha wakulima amesema ameridhishwa na ushindi alioupata mgombea wa CCM na amempongeza, kwa ushindi huo '' Mara zote mtu unaposhindana lazima mmoja ashinde, asiyekubali kushindwa siyo mshindani'' alisema Abdul

Mwajuma Notey mgombea kutoka (UMD) amewapongeza wanaliwale kwa kufanya maamuzi yao na amesema anayaheshimu, amempongeza mbunge mteule kwa ushindi huo ."Nakupongeza sana kwa ushindi ila namkumbusha tu awakumbuke wapiga kura wako wote waliomchagua na wasiomchagua wote ni wapigakura wako" 
Mchakato wa kumtafuta mbunge wa Jimbo la Liwale ulianza mwezi mmoja uliopita ambapo waliotangaza nia ya kuwania kiti hicho ni wagombea kutoka vyama vifuatavyo AAFP kura 18 sawa 0.2% (UMD 109 sawa 0.49% ACT 285 sawa 0.79%CUF 5207 sawa na 12. 92%.
Msimamizi wa uchaguzi mdogo Jimbo la Liwale Luiza Mlelwa akimkabishi chetu mbunge mteuliwa wa Jimbo la Liwale Zuberi Kichauka. Picha na Vero Ignatus
Wa pili kutoka kulia ni Msimamizi wa Uchaguzi mdogo Jimbo la Liwale Luiza Mlelwa akiniandaa kumtangaza mshindi wa kigi cha ubunge Jimboni hapo. 
Mbunge Mteule wa Jimbo la Liwale akionyesha cheti alichokabidhiwa na msimamizi wa uchaguzi mara baada ya kutangazwa rasmi. Picha na Vero Ignatus

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...