Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


KATIKA jitihada za kuijengea Jamii uelewa na hamasa juu ya umuhimu wa kutunza afya na Kufanya Mazoezi, Kampuni ya E World (Events World) kwa kushirikiana na wadau mbali mbali inawaletea mbio za Kigamboni International Marathon, mbio hizi zitaambatana na zoezi la Upimaji wa afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo huazimishwa tarehe 1 mwezi wa 12 kila mwaka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Ndg. Dimo Debwe Mitiki Mwenyekiti wa mbio hizo ambaye pia ni kocha wa michezo ya riadha na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Riadha ya Walemavu Tanzania alisema, Lengo kuu la “Kigamboni International Marathon” ni kuchochea shughuri za kiuchumi kwa kutangaza fursa za uwekezaji,Biashara na vivutio vya kitalii Vilivyopo Kigamboni na maeneo ya karibu, Kuimarisha Afya pia Kuhamasisha michezo ya Riadha kwa maendeleo ya Taifa letu.

Aidha “Kigamboni Marathon” inafanyika kuunga mkono kampeni ya Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha Watanzania kufanya mazoezi ili kuimarisha afya.

Pia Kwa siku za hivi karibuni Tumeshuhudia Viongozi wetu wakihamasisha wafanyabiashara na wadau mbali kuwekeza ndani ya wilaya yetu mpya ya kigamboni, hivyo ni imani yetu kuwa kufanyika kwa „kigamboni International Marathon‟ kutawavutia watu mbali mbali kufika Kigamboni na kujionea uzuri pamoja na fursa zilizopo kigamboni.

Muandaaji wa Mashindano ya Riadha ya Kimataifa ya Kigamboni Dimo Debwe akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wa kutambulisha Mbio hizo zitakazo fanyika Desemba 2 Mwaka hu kuanzia eneo la Fun City Mpaka Daraja la Kigamboni.

Mmoja wa Wafadhili wa Mashindano ya Riadha ya Kimataifa, Sunil Rodrigues akieleza kwanini mbio hizo zitafanyika katika eneo la Fun City Kigamboni.

Mratibu wa Masuala ya Habari wa Mbio za Kigamboni, mwani Nyangasa akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya ushiriki wa Wanahabari Kumi katika Mashindano hayo.

Uongozi wa Mashindano ya Riadha ya Kigamboni Marathoni wakionyesha Flana zitakazotumika katika Mbio za Kigamboni Intenational Marathon.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...