Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kukamatwa kwa Mfanyabiashara, Shabani Hussein maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto ya Ng'ombe, baada yakushindwa kufika Mahakamani bila kutoa taarifa. 

Hati hiyo ya kukamatwa imetolewa leo Oktoba 24.2018 na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Maira Kasonde, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa huyo kushindwa kutokea mahakamani. 

Aidha Hakimu Maira ametoa barua ya wito kwa wadhamini wa mshtakiwa huyo kufika mahakamani na kueleza alipo mshtakiwa. 

Kabla ya kutolewa kwa amri hiyo ya kukamatwa kwa mshtakiwa, wakili wa Serikali, Mosia Kaima, alidai kuwa, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa lakini mshtakiwa hayupo n ahata mashaidi wake pia hawapo. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 12. 2018 kesi hiyo itakapokuja kwa kutajwa. 

Ndama anakabiliwa na mashtaka matano yakiwemo ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, 

Mshtakiwa anadaiwa kughushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

Pia anadaiwa kughushi kwa kutengeneza hati ya kibali ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonesha kilogramu 207 za dhahabu kutoka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...