MAMA, Leo hii unatimiza miaka tisa (9) tokea ulipotuacha hapa duniani. Kila siku tunakukumbuka Mama. Umetufundisha kukua katika upendo, ukweli, uaminifu na kumcha Mungu. Tunamuomba Baba Mungu atuwezeshe tuyaendeleze na kuyaenzi mema yote uliyotufundisha na tuyaendeleze kwa vizazi vyetu vijavyo. MAMA, daima tutaendelea kujivunia zawadi tuliyopewa na Baba Mungu ya maisha yako kwetu sisi kwa maana uliyagusa maisha yetu kwa njia ya pekee.
Unakumbukwa daima na mume wako mpenzi Mzee Lawrence Shelukindo Saguti, watoto, wakwe na wakamwana, wajukuu na vilembwe
...........Tunaendelea kusimama imara na neno toka Ufunuo wa Yohana 12: 11
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
..........Na tukimsifu Mungu tukiimba:
Amini Bwana awapenda, Amini,atawabariki, Atawahurumia wote, wamjiao yeye.
Kweli tutaona furaha, Tukifika kwenye Raha kuu, Tukisafishwa mioyo yetu na Yesu Mwokozi.
Endelea kupumzika kwa amani MAMA!
AMEN



Hakika miaka mingi imepita kumbe tayari miaka 9 Mungu azidi kuwabariki na muendelee kumtumikia yeye, Familia yetu itamkumbuka sana Marehemu Mama Saguti. Apumzike kwa Amani.
ReplyDelete