Na Catherine Francis, Mahakama Kuu - Arusha
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu- Kanda ya Arusha, Mhe. Mosses Mzuna,
amewakumbusha Mahakimu kutekeleza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha haki
inatendeka kwa kila mwananchi na kwa wakati.
Akiwa ziarani Mahakama ya Wilaya Mbulu, Mhe. Jaji Mzuna aliwakumbusha
Mahakimu wilayani humo kuwa wanapaswa kutoa adhabu kwa kuzingatia ukubwa
wa kosa lenyewe na si kwa kuhamasishwa na hisia juu ya kesi husika.
“Wajibu wa kila Hakimu ni kuhakikisha haki inatendeka na kupitia mwenendo
wa shauri na maamuzi yaliyotolewa kabla hawajaruhusu jalada kwenda kwenye
ngazi nyingine za Mahakama,” alisistiza Mhe. Mzuna.
Aidha; Mhe. Jaji Mfawidhi alisisitiza juu ya umuhimu wa taarifa za mashauri
kufikia wadaawa kwa wakati unaostahili ambapo mwenendo wa shauri pamoja na
nakala ya hukumu vinatakiwa viwafikie wadaawa kwa wakati.
Mhe. Mzuna alisema endapo taarifa hizi zitawafikia Wadaawa mapema
zinawawezesha kufanya hatua nyingine kama watakuwa hawajaridhishwa na
maamuzi ya Mahakama hiyo.
Katika kusititiza hilo Mheshimiwa Jaji Mzuna alifanya ukaguzi mdogo wa
majalada ya mashauri yaliyokamilika ili kuweza kugundua ni kwa jinsi gani
Mahakimu wamekuwa wakitekeleza wajibu wao.
Ukaguzi huo ulihusisha majalada ya Mahakama ya Wilaya Mbulu na majalada ya
Mahakama ya mwanzo Endagikot. Pia aliwapa maelekezo na mapendekezo pale
alipogundua kuna changamoto katika kutekeleza wajibu wao.
Katika ziara hiyo, Mhe. Jaji Mfawidhi alikutana pia na Wazee wa Baraza wa
Wilaya ya Mbulu ili kuweza kuwafahamu na kujua changamoto wanazokabiliana
nazo ambazo zinakwamisha ufanisi wa kazi zao.
Jaji Mzuna akikagua majalada ya Mahakama ya mwanzo ya Endagikot
wilayani Mbulu.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...