NA AHMED MAHMOUD, ARUSHA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa
anatarajiwa kufunga maadhimisho ya tamasha la mwezi wa Urithi wa
Utamaduni mkoani hapa

Akizngumza na waandishi wa habari Jijini hapa jana na kaimu mkuu wa
mkoa wa Arusha Theresia Mahongo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya
Karatu, maadhimisho hayo yatafanyika wilayani Karatu kuanzia Oktoba
nane mwaka huu.

Alisema maadhimisho hayo ambayo yalizinduliwa Jijini Dodoma Septemba
15 mwaka huu na makamu wa rais Samia Suluhu Hassan yaliendelea
kufanyika maeneo mbalimbali nchini ikwemo Zanzibar,Mwanza na Dar es
Salaam.Alisema kabla ya kilele hicho maadhimsho hayo yatafanyika kwa siku tano kuanzia Oktaba nane hadi 12 wilayani Karatu kwenye viwanja vya
mazingira ambapo yatakwenda sambamba na maonyesho mbalimbali ya
kiutamaduni.

“Maadhimisho haya yenye jina la “Urithi Festival Celebrate our
Heritage kimkoa yataanza kuadhimishwa wilayani Karatu kuanzia Oktoba
8 mwake na kilele cahek kitakuwa Oktoba 13 mwaka huu katika uwanja wa
Sheikh Amri Abeid uliopo Jijini Arusha”.

Aliongeza”Maonyesho hayo yatashirikisha ngoma za makabila 10 ya mkoa
huu,maigizo,kutembelea vituo mbalimbali vya utalii pamona na michezo
mbalimbali ya asili”

Licha ya maonyesho hayo pia wananchi wa mkoa wa Arusha watapata fursa
ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii kitamaduni ikwemo
makumbusho mbalimbali na bonde la Ngorongoro kwa gharama ndogo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...