Mwandishi Wetu, Calabar
Mnenguaji nyota wa muziki wa dansi nchini Hassan Mussa 'Super Nyamwela'leo anatarajia kuliongoza kundi lake binafsi la Ubuntu (Ubuntu Tradional Band) katika tamasha la kimataifa la utamaduni litakalofanyika nchini Nigeria katika mji wa Calabar nje kidogo ya jiji la Abuja.
Hii ni mara ya pili kwa Nyamwela na bendi yake ya Ubuntu kushiriki tamasha hilo ambalo linashirikisha nchi zaidi ya 60 duniani.
Kwa Tanzania ni Ubuntu pekee ndiyo imepata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka kwa udhamini wa serikali ya Nigeria ambayo imekuwa ikilitumia kutangaza utalii wa nchi yake.
Tangu kuwasili kwa Ubuntu mjini Calabar, hofu imeanza kutanda kwa makundi mengine wapinzani wake ambayo mwaka jana yalishindwa kufua dafu mbele ya Nyamwela na wenzake.
Tamasha hilo lilianza rasmi Desemba 4 mwaka huu na linatarajia kufikia tamati Januari 4 mwaka 2019.
Wasanii wa Bendi ya Utamaduni ya Ubuntu (Ubuntu Traditional Band), ikiongozwa na Hassan Mussa maarufu Super Nyamwela, katika picha ya pamoja wakijiandaa kutumbuiza katika Tamasha la Kimataifa (Calabar Carnival Festival) linalofanyika Mjini Calabar, nchini Nigeria jana. Picha na Esther Mbussi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...