Kwa mwaka 2018 Mahakama ya watoto ya Kisutu ilipokea jumla ya mashauri
118 ya jinai na makosa 295 ya madai yalipokelewa na kufanyiwa kazi na
matukio ya kesi za watoto yakiwa wengi wa watoto hao ni wale ambao
wamekinzana na Sheria na pili ni wale ambao Sheria inawakuta na
makosa.
Hayo yamebainishwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya
Kisutu Bi. Agness Mchome wa jijini Dar es Salaam wakati akitoa maelezo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu alipotembelea
katika Mahakama ya Watoto Kisutu jijini Dar es Salaam.
Hakimu Agness Mchome amewataka wazazi kutimiza wajibu wao wa malezi
kwa watoto ili kuwaepusha na mashitaka yanayozuilika kwani watoto
wanaofikishwa mahakamani ni wale ambao wazazi au walezi wao
hawakutimiza wajibu wao wa kutoa malezi stahiki.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu ameridhishwa na utendaji kazi
wa Mahakama ya Watoto ya Kisutu jijini Dar Es Salaam kwani imekuwa
ikifanya kazi nzuri ya kusaidia kurekebisha maadili ya watoto nchini.
Dkt. Jingu amesisitiza wazazi kuzingatia malezi bora na kutoacha
watoto kuangalia televisheni na mitandao ya kijamii wakati wote ambapo
kwa kiasi kikubwa mitandao ya kijamii na video zisizo na maadili
zinachangia kuharibu maadili ya watoto nchini.
Katibu
Mkuu Wizara yaAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara
kuu ya Maendeleo ya Jamii) (kushoto) Dkt. John Jingu akisisitiza jambo
wakati wa ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa kazi za Maendeleo na
Ustawi wa Jamii na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Mkoa
Dar es salaam (katikati) ni Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Bi. Rehema
Kombe na kulia ni Afisa Ustawi wa Jamii wa mkoa wa Dar es Salaam Bi.
Sufiani Mdolwa.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Given Sure
(kulia) akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa kazi za Idara ya
Maendeleo ya Jamii ya Mkoa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii)
Dkt. John Jingu (hayupo pichani) na kulia ni Afisa Ustawi wa Jamii wa
mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sufiani Mdolwa.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...