Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Bukoba .
Mkutano wa Wadau wa Bomba la Mafuta litakaloanzia Nchini Uganda mpaka Jijini Tanga hapa Nchini Umefunguliwa rasmi na Waziri wa Nishati Medard Kalemani (MB) ambapo masuala mbalimbali yamejadiliwa, yakiwemo yale yanohusu Fursa katika maeneo ya mradi pamoja na namna ya kulinda mradi.
Kikao hicho kilichofanyika mapema June Mosi, 2019 katika Ukumbi wa E.L.C.T Mjini Bukoba kikihudhuriwa na Viongozi kutoka Wizarani, na Mkoani, lengo hasa likiwa ni kujadili namna ya Uharakishaji wa Ujenzi wa Bomba la mafuta litakalokuwa na urefu
Likipitia Mikoa minane ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Singida, Dodoma Manyara, Arusha na Tanga huku mlango Mkuu ukiwa ni Mkoa wa Kagera.
Akizungumza kabla ya kufungua Mkutano huo, Waziri wa Nishati Mhe. Medard Kalemani amesema kupitia Bomba hili la Mafuta Wanakagera wana nafasi kubwa kuchangamkia fursa katika maeneo yao ambapo Bomba hilo litapitia zikiwemo fursa za kazi za Vibarua, kuuza Chakula, huduma ya Malazi n.k huku masuala mengine yakitaalamu yatachukuliwa na Watanzania wote kulingana na uhitaji, huku jumla ya Ajira zaidi ya Elfu kumi zikitarajiwa kutolewa.
Aidha wakati akijibu Hoja mbalimbali ikiwemo hoja ya Vijiji ambavyo bado havijafikiwa na Umeme Waziri Kalemani amesema Ni lazima Vijiji hivyo vifikiwe Umeme kwanza mapema na haraka iwezekanavyo kabla ya Ujenzi wa Bomba la Mafuta, na pale itakapobidi REA wasaidiwe na TANESCO ili mradi usikwame lengo likiwa ni kukamilisha Ujenzi wa Bomba kwa wakati na ikibidi kabla ya Wakati.
Ujenzi wa Bomba hili la Mafuta utakaoanza Mwezi Septemba Mwaka huu Linaloanzia Nchini Uganda Urefu wa kilometa 298 na Urefu Kilometa 1147zitakuwa Nchini Tanzania, kwa Mkoa wa Kagera likipita Wilaya za Missenyi, Bukoba Vijijini na Muleba lenye Urefu wa Km. 1445 Kati ya Pumping Station moja itakuwa Kagera, Kati ya Kambi 12, mbili zitakuwa Kagera. Mkutano huo ni mwanzo wa Mkutano mingine mikubwa na midogo ambayo itajadili namna ya Utekelezaji wa Mradi huo.
Pichani ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akitoa salaam zake wakati wa ufunguzi wa Mkutano kujadili utekelezwaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Mkoani katika Ukumbi wa E.L.C.T Kagera
Pichani ni Mshiriki wa Mkutano Ndg. Runyogote M/kiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa akitoa ushauri wake juu ya ufanisi wa Mradi wa Bomba la Mafuta.
Pichani ni Viongozi pamoja na washiriki wa Mkutano wakiendelea kumsikiliza muwezeshaji (hayupo pichani) wakati akiendelea kuwasilisha mada yake juu ya mradi wa Bomba la Mafuta
Pichani ni Profesa Anna Tibaijuka (MB) jimbo la Muleba Kusini ambapo pia Bomba litapitia akitoa mchango wake wakati wa mjadala wa Bomba la mafuta.
Pichani ni Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu wakati akizungumza na wadau waliohudhuria Mkutano wa Kujadili Uharakishwaji wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Mjini Bukoba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...