Kikundi cha NGUVUKAZI kilichopo Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli Musoma Vijijini mkoani Mara,kilianzishwa Mwaka jana (2018) wakiwa chini ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Jamii (PCI, Project Concern International) lililowapa MAFUNZO ya KILIMO Wanachama wa Kikundi hicho na baadae wakaanzisha KILIMO cha MAHINDI, VIAZI LISHE, na MPUNGA.

Afisa Kilimo wa Kata, Ndugu Sevas Ngova ameeleza kwamba Kikundi cha NGUVUKAZI kilipata MAFUNZO ya ZAO JIPYA JIMBONI la ALIZETI na baada ya MAFUNZO walianza na SHAMBA DARASA kwa kutumia Mbegu walizopewa na Mbunge wa Jimbo,  Profesa Sospeter Muhongo. Mavuno ya awali ya ALIZETI yalikuwa ya MAGUNIA 10. Mbegu nyingine walizopokea kutoka kwa Mbunge wao huyo ni za MTAMA, MIHOGO na UFUTA.

Ndugu Tore Masamaki, Mwenyekiti wa Kikundi cha NGUVUKAZI ameeleza kwamba Kikundi hicho kilianza na WANACHAMA 18 na baada ya MAFANIKIO ya kuridhisha kupatikana, Wanachama wameongezeka na kufikia 30 (thelathini).

Kikundi cha nguvu kazi kinaendelea kushirikiana na Shirika la PCI ambalo moja ya malengo yake makuu ni kutoa CHAKULA mashuleni, ikiwemo Shule ya Msingi Bwenda.

"Kupitia Kikundi hiki mavuno yanayopatikana hupelekwa shuleni hapo, na mengine ni kwa manufaa yao wenyewe na familia zao , Masamaki aliyasema haya na kuongeza kwamba sasa wanatafuta vifaa vya umwagiliaji waanze Kilimo hicho.

Mwalimu Mkuu  Bwenda, Christopher Cosmas  amekiri kupokea jumla ya KILO 220  za MAHINDI kutoka Kikundi cha NGUVUKAZI  kwa ajili ya CHAKULA cha WANAFUNZI.

Mwalimu Mkuu huyo anasema CHAKULA kinachotelewa kwa WANAFUNZI wote hapo Shuleni kimefanya UTORO usiwepo na HAMASA ya Wanafunzi kupenda kupata ELIMU imeongezeka.

Aidha Diwani wa Kata ya Rusoli, Mhe Boaz Nyeura ameshukuru Kikundi cha NGUVUKAZI kwa jitihada zake na kupitia vikao vya hadhara ameomba VIKUNDI vingine kujitokeza kusaidia UPATIKANAJI wa CHAKULA kwa Shule nyingine ndani ya Kata yao ya Rusoli.
 Wana Kikundi cha NGUVUKAZI wakiendelea na shughuli ya kuandaa mahindi yao yakauke vizuri mara baada ya kuvunwa shambani kwa ajili ya kutoa msaada mashuleni.
 Kikundi cha NGUVUKAZI kikiwa na mavuno ya MAHINDI kutoka shambani mwao wakiwa sambamba na Diwani wao, Mhe Boaz Nyeura (aliyevaa nguo za Chama- CCM) 
 Diwani wao, Mhe Boaz Nyeura (aliyevaa nguo za Chama- CCM)  kizungumza na Kikundi cha  NGUVUKAZI  Kijijini Buanga, Kata ya Rusoli,Musoma mkoani Mara 
 Kikundi cha NGUVUKAZI kikiwa na mavuno ya MAHINDI kutoka shambani mwao. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...