Hussein Stambuli, Morogoro
SERIKALI mkoani morogoro imewachukulia
hatua baadhi ya watumishi wa sekta ya afya kwa kuwahamisha vituo baada ya
kukithiri kwa malalamiko ya tuhuma za rushwa, lugha chafu na utendaji mbovu
akiwemo Mganga Mkuu na Muuguzi Mkuu wa Mkoa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari,Katibu
Tawala Mkoa wa Morogoro Cliford Tandari
amesema uhamisho huo utahusisha Mganga mkuu wa mkoa, Muuguzi Mkuu wa mkoa,
Mganga Mkuu wa meno wa Mkoa pamoja na watumishi wa idara mbalimbali zilizopo
katika sekta hiyo.
"Kufuatia ziara ya Naibu Katibu
Mkuu TAMISEMI Dk.Gwajima baada ya kufanya ukaguzi katika halmashauri zote mkoani
hapa sasa imebainika kumekuwa na viashiria vya rushwa, hali mbaya ya utoaji
huduma kwa wagonjwa, majibu mabovu yanayotolewa na wauguzi.
"Sisi kama Serikali tumeamua
kuingia kati suala hili na kuhakikisha huduma za afya mkoani hapa zinatolewa
kwa usawa, haki na uboraa,"amesema Katibu Tawala huyo.
Watumishi hao watapangiwa maeneo
mengine ya kazi nchini huku Serikali ikiahidi kufuatilia mwenendo wao wa kazi
mahali popote watakapokuwa kwani lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma
wanakuwa msaada mkubwa kutatua kero za wananchi.
Katibu tawala mkoa wa morogoro, Cliford Tandari akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro kuhusu watendaji wa sekta ya afya ya mkoa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...