Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
WATANZANIA wametakiwa kuwa na tabia ya kuwaasili watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto wanaoishi mazingira magumu ili waweze kuwasaidia watoto hao.
Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi wa Kituo cha Samaritan ambacho kinajuhusisha na kulelea watoto yatima na wale waliotelekezwa na wazazi wao Father Josephaty Mmanyi wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea zawadi za ya vyakula kwa Sikukuu ya Iddi kutoka Kampuni ya Promasidor wanaotengeneza maziwa ya Cowbell.
Father Mmanyi amesema kuwa ni vema Watanzania wakajenga tabia ya kusaidia kwa kuwaasili watoto (kuwadapti) wanaoishi vituoni ili nao wajisikie vyema na wajione wanandugu na wazazi kama walivyo watoto wengine.
"Unajua hawa watoto ni binadamu na wao wanahitaji malezi ya wazazi kama vile wengine wanavyohitaji, hivyo tunawaomba wananchi kwa ujumla tujitokeze kuwaasili watoto hawa ili nao wasikae vituoni muda mrefu ,maana pia jinsi wanavyokaa mda wanazidi kuwa wapweke zaidi,"amesema.
Aidha amebainisha hadi sasa jumla ya watoto watano wameshaasiliwa ambapo kati ya hao watatu wameasiliwa nje ya nchi ya nchi na wawili ndani ya nchini ambapo sheria zote za Serikali zimefuatwa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo pamoja na chakula ,Meneja Masoko wa Kampuni ya Promasidor Vitus Mpanda amesema kuwa hiyo si mara yao ya kwanza kutoa msaada wa aina hiyo kwani wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara pamoja na kufanya shughuli za kijamii.Wametoa msaada wa mchele, sukari, unga na mafuta ya kula.
Amesema nia ya kutoa vitu hivyo ni kurudisha fadhila kwa wananchi na jamii kwa ujumla kwani wananchi wamekuwa wakinunua maziwa yao na bidhaa zao, hivyo wameona warudishe fadhila kwa kuwapatia watoto msaada wa vyakula na zawadi nyingine.
"Tunataka watoto hawa washerekee iddi vizuri kama watoto wengine, pia tunaamini kuwa kwenye kutoa ndipo mungu anatubariki vyema,"amesema na kutoa mwito kwa wananchi kuendelea kuendelea kusaidia yatima,"amesema.
Meneja masoko wa kampuni ya Promasidor kampuni inayozalisha maziwa ya cowbell Vitus Mpanda akimkabidhi mkurugenzi wa wa kituo cha Samaritan zawadi za iddi
Mkurugenzi wa kituo chakulelea watoto yatima pamoja na Wale waliotelekezwa na wazazi wao Samaritan father, Josephaty Mmanyi akizungumza na Waandishi wa Habari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...