Na.Khadija seif,Globu ya jamii
WANAMUZIKI wa bongofleva waasa kuacha kufanya mzaa na dini ya kiislam.
Akizungumza na michuzi tv muimbaji wa qaswida Masoud ferouz amesema si vizuri kwa wasanii kuamua kuimba qaswida na baadae kurudi kwenye miziki ya kidunia (bongofleva).
"Wapo wasanii ambao wanafanya miziki ya aina nyingi hasa ya kidunia ,ni sawa kutokana na wote tunatafuta ridhiki ni kheri ukafanya muziki wa aina moja na kujua shabiki zako kwa urahisi,"
Aidha ,ameweka wazi kuwa kundi la qaswida la nasaha lipo kwa ajili ya kuburudisha, kufundisha na kuwa mchamungu kutokana na tungo na uimbaji wake wa kipekee."Kundi hili linabeba waimbaji takribani 11 akiwemo Mariam hamdun ambae anafanya vizuri katika soko la muziki wa qaswida nje na ndani ya nchi,"
Pia amewaomba wapenzi na mashabiki wa nasaha kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la pili la usiku wa furaha (laylatul helwa) juni 16 katika ukumbi wa Daimond jubilee jijini Dar es salaam."Siku hiyo ya tamasha utakua ni usiku wa kitofauti kwani waimbaji wengine wapya watatambulishwa ambao tayari wapo kwenye muziki wa mwambao,"
Kwa upande wake Mariam hamdun amesema sababu inayopelekea kupata mashabiki wengi ni sauti yake ya kipekee sana huku nidhamu ikiwa ndio nguzo kubwa kwa Msanii yoyote yule.
"Vyombo tunavotumia katika qaswida zetu ni vya kiasili kama zumari,kinanda na filimbi na hata video zetu tunatumia mandhari ya kiasili bahari,makumbusho ya kale na vitu mbali mbali ambavyo vilitumika kwenye qaswida ya utu,algenani mahaba ya mtume.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...