Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

WAFANYABIASHARA ndogondogo zaidi ya 17 waliopo Soko kuu la mjini
hapa,wameulalamikia uongozi wa Halimashauri ya jiji la Arusha,kwa
kutowarejesha katika maeneo yao waliyokuwa wanafanyia biashara awali
ambapo kwa sasa wanataka kuyagawa kwa wafanyabiashara wengine.


Wakizungumza na baadhi ya wafanyabiashara hao,Nelson
Alfayo,Gilbert Fransis,Joseph Mungaya,juma Zuberi na Gasper
Ngowi,wamesema kuwa wameshangazwa na uamuzi wa uongozi wa halimashauri ya jiji kwa uamuzi huo kwani wao wamekuwa wakifanya biashara katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 40 sasa.

Wamesema kuwa uongozi wa jiji la Arusha uliwaamuru wapishe eneo hilo
ili waweze kujenga mabanda ya kisasa ndani ya soko hilo kwa ahadi kuwa
mara baada ya kukamilika wao watapewa kipaumbele kurejeshwa katika
eneo hilo jambo ambalo halijafanyika.

Mmoja wa wafanyabiashara hao,Nelson Alfayo,alisema kuwa uongozi wa
jiji uliwaambia waandike barua ya kuomba kugawiwa maeneo hayo jambo
ambalo walilifanya kwa kuandika barua hiyo mei 13, lakini cha
kushangaza hadi leo hii wamekuwa wakipigwa danadana ikiwa ni pamoja na kupewa vitisho vya mara kwa mara.

“Baada ya kuandika barua tumekuwa tukifuatilia na kwa mara ya mwisho
tuliambiwa turudi tarehe 29 Mei ambapo tulifanikiwa kukutana na
mkurugenzi Mtendaji wa Jiji Dk.Ahmad Madeni lakini tulishangazwa na
kitendo chake cha kuamuru Mwenyekiti wetu Fredy Eliphace na baadhi ya
wenzetu watatu kukamatwa na kufikishwa kituo cha polisi”alisema
Alfayo.

Aliongeza kuwa wenzao walipopelekwa polisi walifunguliwa jalada la
kufanya biashara bila leseni jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote
kwani walikuwa nazo pamoja na vitambulisho vya mjasirimali ambapo
walilazimika kulala katika kituo kikuu cha polisi hadi kesho yake
walipotoka kwa dhamana.

Amesema kuwa kitendo cha kutishiwa maisha na wenzao kukamatwa kimekuwa kikiwapa hofu kubwa sana kuendelea kufuatilia majibu ya barua yao ambapo wameziomba mamlaka za juu kuliangalia suala hilo na kuhakikisha linapatiwa ufumbuzi.

Akizungumzia suala hilo Mstahiki Meya wa jiji la Arusha,Kalist
Lazaro,alisema kuwa wafanyabiashara hao wanatakiwa kufuata taratibu
stahiki za kuomba kupatiwa eneo la kufanyia biashara ambapo baada ya
kutuma maombi wanatakiwa wasubiri vikao husika vikae kwa ajili ya
kuwajadili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Arusha.Dkt Ahmad Madeni
alinukuliwa aakiwaambia wafanyabiashara hao kuwa endapo wanataka
kuomba maeneo ya kufanyia biashara ndani ya jiji wanatakiwa kuomba mtu
moja moja na sio kuomba kama kundi kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na
fujo.

Naye Afisa Biashara wa jiji la Arusha,Godfrey Edward ameliambia gazeti
hili kuwa ni kweli wafanyabiashara hao walifika katika ofisi za
halimashauri hiyo kuomba wapatiwe maeneo hayo,lakini halimashauri
imetenga maeneo hayo kuwapatia wafanyabiasha ambao walikuwa na
migogoro ya vibanda vya biashara kwa muda mrefu katika maeneo ya
biashara yanayomilikiwa na halimashauri ya jiji hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...