Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Bodi ya Mikopo ya Wananfunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imepanga kutoa mikopo yenye thamani ya Sh. Bilioni 450 kwa wanafunz 128,285 katika mwaka wa masomo 2019/2020.

Akizungumza na waandishi Habari katika Maonesho ya Vyuo Vikuu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Afisa Habari Mwandamizi  wa Bodi hiyo Veneranda Malima amesema kuwa kati ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza watakuwa 45,000.

Amesema mwaka wa bajeti  2018/2019 bajeti iliyokuwa imepangwa ilikuwa ni sh.Bilioni  427.7 kwa kusomesha wanafunzi 123,000, kati yao wanafunzi wa mwaka wa kwanza walikuwa 41885.

Malima amesema kuwa kuna ongezeko kubwa na kutaka wanafunzi wafuate taratibu za Uombaji wa mikopo kwa ajili ya elimu ya juu.

Amesema wako katika maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu pamoja na kujibu changamoto za wanafunzi katika Uombaji wa mikopo hiyo.

Aidha amesema kwa walionufaika na mikopo  urejeshaji umezidi kuongezeka na kutaka kuendelea kurejesha kwa ajili ya kunufaisha wengine.
 Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Veneranda Malima akizungumza na waandishi habari katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wakipata maelezo kwa Afisa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kuhusiana na Uombaji wa mikopo ya elimu ya Juu katika Bodi hiyo katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakipata maelezo kutoka Kwa maafisa Bodi katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...