Mratibu Taifa wa Programu ya Ubia wa Kilimo Tanzania chini ya
Baraza la Kilimo Bw. Mark Magila akifungua Warsha ya siku moja iliyofanyika
Mkoani Morogoro na kujumuisha Wadau wa Kilimo ilikujadili matokeo ya Utafiti
kuhusu Mfumo wa uagizaji Mbolea kwa Pamoja.
Makamo Mwenyekiti wa Chama cha wasambazaji wa Pembejeo nchini
TADCOS Bw. Iddi Madeni akichangia kuhusu Mfumo huo wa uagizaji wa Mbolea kwa
pamoja, ambapo pamoja na masuala mengine amesema ni muhimu serikali ikawa
inawashirikisha kabla ya upangaji wa bei elekezi .
Mkulima wa Tumbaku kutoka Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Bw.
Juma Phesto akichangia mada kuhusu uagizaji wa Mbolea kwa pamoja ambapo amekiri
kuwa mfumo huo umesaidia mbolea kuwafikia wakulima kwa wakati, Mkutano huo
umefanyika Mkoani Morogoro.
Sehemu ya washiriki wa Warsha hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada katika mkutano huo uliofanyika Mkoani Morogoro.
Washiriki wa Warsha ya wadau wa Kilimo iliyofanyika Mjini Morogoro
na kuratibiwa na Baraza la Kilimo Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara
baada ya kumalizika kwa warsha hiyo.
SERIKALI imeelezea kuridhishwa na mfumo wa
uagizaji wa Mbole kwa pamoja licha ya uwepo wa changamoto kadhaa zikiwemo za
ucheleweshaji wa mbolea kuwafikia wakulima ikiwa ni pamoja na suala la bei
elekezi.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa jana Mjini Morogoro na Afisa
Kilimo Idara ya Mazao Kitengo cha Pembejeo kutoka Wizara ya Kilimo Bw Joseph
Lyafwila wakati wa Warsha ya wadau wa Sekta ya Kilimo iliyokuwa ikiangazia
matokeo ya utafiti uliofanywa kuhusu Mfumo wa uagizaji wa Mbolea kwa Pamoja
ulioandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.
“Kwetu kwenye Sekta ya Kilimo Mfumo huu ni mpya na
tayari tumeona mafanikio yake ndani ya
kipindi cha miaka mitatu, hivi sasa Mbolea inafika nchini kwa wakati na
wakulima pia inawafikia kwa wakati na kama nilivyosema ni ukweli kwamba bado
kunachangamoto kadhaa,
“Tunajua pia wakulima wamekuwa wakilalamikia suala la bei na
hii inatokana na ukweli kwamba kuna baadhi ya vijiji viko mbali sana na
inafanya bei inapanda kidogo inagwa Serikali bado inangalia changamoto
zote zinazoendelea kujitokeza katika
mfumo huu ili tuweze kuzishughulikia “ alisema Bw Joseph.
Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utetezi kutoka Baraza la
Kilimo Tanzania Bw. Timothy Mmbaga alisema kuwa waliamua kufanya utafiti huo
kuhusu maendeleo ya mfumo ili kuona namna inavyoweza kuishauri Serikali namna
bora zaidi ya kuendelea na mfumo huo.
“Kabla ya mfumo huu kulikuwa na changamoto nyingi sana watu
walikuwa wanauziwa mbolea feki wengine walikuwa wanauziwa hadi siment, lakini
Baraza la Kilimo tulipiga sana kelele na tunaishukuru Serikali ililiona hili na
hatimaye kuja na mfumo huu,
“Tunajua mahitaji ya mbolea kwa sasa yanazidi kuongeka hivi
sasa inakadiriwa kufikia tani laki nne ingawa kupitia mfumo huu ni tani 70,000
pekee ndio inayoagizwa ingawa tunajua kuna njia nyingine nyingi za uagizaji wa
mbolea zaidi ya DAP na UREA zinazoagizwa kupitia mfumo huu” alisema Bw. Mmbaga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...