Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janet Bitegeko akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa kilimo ilikujadili ushiriki wa Sekta Binafsi katika utekelezaji ASDP II, pamoja na masuala mengine amesema Baraza la Kilimo litaendelea kuwasemea wakulima.
Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo Tanzania Bw. Enock Ndondole akichangia wakati wa mkutano huo wa wadau wa Sekta ya Kilimo, Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania na kufanyika Mjini Morogoro
Mratibu wa Ubia wa Kilimo Kanda namba 4 chini ya Baraza la Kilimo Tanzania BI Mwajuma Sizya akichangia katika warsha ya wadau wa kilimo ilikuona ushiriki wao katika utekelezaji wa Mpango wa ASDP II, Mkutano huo umefanyika Mkoani Morogoro.
Mratibu wa Ubia wa Kilimo Kanda namba 4 chini ya Baraza la Kilimo Tanzania BI Mwajuma Sizya akichangia katika warsha ya wadau wa kilimo ilikuona ushiriki wao katika utekelezaji wa Mpango wa ASDP II, Mkutano huo umefanyika Mkoani Morogoro.
Na Mwanandishi wetu.
WADAU wa Sekta Binafsi nchini wamesema Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili ASDP II bado kunachangamoto nyingi za ufanyaji biashara ikiwa ni pamoja na uwepo wa matamko yanayozui usafirishaji wa mazao nje ya nchi.
Wakizungumza wakati wa Warsha ya kujadili ushiriki wa Sekta Binafsi katika utekelezaji wa ASDP II iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania na kufanyika jana Mkoani Morogoro wamesema ni muhimu Mpango huo ukawa jumuishi si tu kwenye makaratasi, bali iwe jumuishi kwenye utendaji, maamuzi ya kila siku ya kisera ili sekta binafsi iweze kushiriki vema zaidi katika Mpango huo.
“Tumekuwa tukiathiriwa sana na matamko mengi hasa ya ufungaji wa mipaka, mfano SUMRI alikuwa na tani 5,000 za Mahindi ghafla likatoka TAMKO la kuzui kuuza nje, unaweza kuona namna tamko la mtu mmoja linavyoathiri saana , unakuta mtu mmoja anatoa tamko ambalo athari yake ni kubwa sana kiuchumi kwa mtu mmoja na jamii nzima.
“Lakini pia unakuta mtu anamkataba wake wa kuuza mazao nje ya nchi katafuta wakulima amewapa Mbolea, Mbegu mwisho wa siku mavuno yanakomaa na muda huo huo unakutana na,
“Tamko la kutokutoa mazao Wilaya moja hadi nyingine, sasa unaona ambavyo mazingira yanavyoiathiri sekta binafsi kwa hiyo ni muhimu changamoto hizi zikafanyiwa kazi vizuri na serikali ili tuweze kushiriki vizuri katika ASDP II” alisema Bw.Joseph Massimba kutoka kampuni ya SUGECO.
“Kimsingi changamoto ni nyingi hasa haya mazuio ya usafirishaji wa mazao nje ya nchi yanaathiri saana, sisi tunategemea masoko ya nje sasa unapozuiwa unajikuta unabaki na mzigo mkubwa sana ambao soko la ndani haliwezi kuumudu mzigo ulipo, lakini pia ni muhimu tuwe tunashirikishwa kama sekta binafsi “ alisema Bi Sifa Gerana ambaye ni Msindikaji wa Bidhaa za Mchele na Mahindi.
Kwa upande wake Mtafiti Mshauri aliyefanya utafiti kuhusu changamoto zinaikabili Sekta Binafsi kushindwa kushiriki kikamilifu katika ASDP II Bw. Apromius Mbilinyi amesema ni wakati muafaka kwa Sekta Binafsi kuanza kuwekeza katika Sekta ya Kilimo kwani kuna fursa nyingi hasa katika uongezaji wa thamani.
“Asilimia 70 ya mbegu zinaagizwa nchi ya nje, hii ni fursa kwa Sekta Binafsi kuwekeza lakini pia lazima wajitokeze kuwekeza katika ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula kwa sababu asilimia 30 ya mazao nchini yanaharibika baada ya kuvunwa kwa hivyo ni muhimu Sekta binafsi ikazitazama fursa hizi” alisema.
Alisema kuwa Sekta Binafsi kwa sasa inachangia asilimia 65 ya ajira na kwamba kupitia asdf ii ajira nyingi zaidi zinaweza kupatikana hasa katika uongezaji wa thamani wa bidhaa za mazao na kusema ni muhimu serikali ikazifanyia kazi changamoto kadhaa zinazoikabili sekta ya kilimo.
Kwa upande wake Afisa Sera Mwandamizi kutoka Baraza la Kilimo Tanzania ambao ndio waandaaji wa Mkutano huo Bi Laetitia Wiliam alisema waliamua kufanya utafiti huo baada ya kuona wadau wengi wa Sekta binafsi wakiwa na ukakasi katika kushiriki katika utekelezaji wa mpango huo ambapo sekta binafsi inatarajiwa kutoa asilimia 59 huku seriklai ikitoa asilimia 41 katika kukamilisha mpango huo.
“Ni kweli ndani ya ASDP II kuna fursa nyingi saana, ila kunavikwazo vya kisheria na kikanuni ambavyo vinaleta changamoto kidogo kiutekelezaji hasa kwa sekta binafsi , lakini sisi kama Baraza la Kilimo Tanzania baada ya mkutano huu tutaandika andiko letu la Kisera ilikuweza kuishauri Serikali ili iweze kufanyia kazi changamoto hizo na tumekuwa tukifanya hivyo na serikaLi imekuwa ikifanyia kazi” alisema Bi Laetitia Wiliam.
Akizungumza katika mkutano huo Mchumi kilimo dawati la ASDP II kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw Militon D.Manyara licha ya kukiri uwepo wa changamoto kadhaa za kiutekelezaji wa ASDP II na kwamba Serikali bado inaendelea kuzifanyia ili kukifanya kilimo kiwe na tija.
“Zaidi ya asilimia 78 ya tozo ambazo wadau wamekuwa wakizilalamikia tayari serikali imekwisha kuzifanyia kazi na kupitia BLUE PRINT tunaamini changamoto nyingi zinazoelezwa hapa zitafanyiwa kazi kikamilifu” alisema Bw. Militon.
“Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto zote inapitia sera na taratibu na kanuni ili kukifanya kilimo kiwe chenye tija na iweze kumsaidia mkulima aweze kunufaika na sekta ya kilimo” alisema.
Mkutano huo wa siku moja uliofanyika mjini Morogoro na kuandaliwa na Baraza la kilimo Tanzania ulihudhuriwa na wadau wote wa sekta binafsi ikiwa ni pamoja na maafisa wa ACT/TAP pamoja na Maafisa kutoka wiraza za kilimo na viwanda na biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...