Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiongoza kikao kazi na Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) (Wa Pili kulia) akiongoza kikao kazi na Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Tume y maendeleo ya Ushirika Dkt Titus Kanani (Wa Pili kulia), Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bi Elizabeth Makwabe (Wa Kwanza Kushoto) na Mrajisi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt Benson Ndiege.
Mwenyekiti wa Tume y maendeleo ya Ushirika Dkt Titus Kanani akizungumza wakati wa kikao kazi cha Tume hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika pamoja na Menejimenti ya tume hiyo mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Dodoma
Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya
Ushirika nchini hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.
Amesema
kuwa Mali zinaibiwa za wananchi, watu wanauziana viwanda huku Ubadhilifu ukiwa
umekithiri kuliko kawaida lakini bado kuna tume ya Maendeleo ya Ushirika.
Mhe
Hasunga ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Makamishna wa
Tume hiyo katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo tarehe 25 Octoba 2019.
Waziri
Hasunga amesema kuwa jumla ya Bilioni 124 zimeibiwa kwenye vyama vya ushirika
lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, "Mnataka mpaka kuwe na posho ndipo
kamati ikutane kuona ulazima wa kusimamia fedha na Mali za ushirika" Alihoji
Mhe Hasunga
Aliongeza
kuwa wizi wa mali na fedha hizo za ushirika ni ishara ya makamishna kutofanya
majukumu yao ipasavyo hivyo jambo hilo linapelekea Wanachama kuendelea
kuteseka.
"Nasikitika
sana Watu walioaminiwa na kupewa dhamana wameshindwa kutekeleza majukumu yao, kwenye
zao la ufuta pekee zimeibiwa Bilioni 2.5 lakini wahusika wanadunda mtaani
kadhalika mazao kama ya korosho na Pamba ambapo hakuna Ushirika badala yake
kuna madalali tu" Alisema
Mhe
Hasunga ameongeza kuwa hakuna sababu ya kuwa na Tume ya Ushirika isiyotekeleza
majukumu yake ipasavyo huku akiongeza kuwa serikali inataka kujenga ushirika
lakini kuna watu kazi yao ni kubomoa, na kuweka urasimu katika utendaji.
Waziri
Hasunga amemtaka Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya ushirika Dkt Titus Kanani
kuchukua hatua za haraka kwa watendaji wote wa Tume hiyo ambao wameshindwa
kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Mhe
Hasunga amesema kuwa endapo ushirika utasimamiwa vizuri wananchi watakuwa na
maendeleo maradufu yatakayopelekea Taifa kuendelea mbele kiuchumi.
Kadhalika
ametoa nafasi ya ziada kwa Tume hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha
matokeo makubwa ya uwajibikaji vinginevyo ametishia kuivunja tume hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt Titus Kamani amempongeza Waziri wa Kilimo kwa kukubali kushiriki katika kikao hicho huku Kamishna wa Tume hiyo Mudhihir M. Mudhihir akizungumza kwa niaba ya Makamishna wengine amehakikisha kuwa Tume hiyo itatekleza majukumu yake kwa weledi mkubwa.
MWISHO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...