Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kutolewa maamuzi kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Yusufu Ali maarufu kwa jina la Mpemba wa Magufuli na wenzake, kwa sababu mawakili wanao wawakilisha ashitakiwa hawapo.
Katika kesi hiyo Mpemba anashtakiwa pamoja na, Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa.
Mapema leo Oktoba 16, 2019 wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa maamuzi na kuendelea na usikilizwaji hata hivyo, alidai mawakili wa washtakiwa hao hawapo mahakamani.
Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 21,(jumatatu) na kusema kuwa, kesi haiwezi kurndela sababu mawakili hawapo hivyo, aliwataka washitakiwa kuhakikisha mawakili wao wanafika siku hiyo.

Washitakiwa hao wanaokabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6 na tayari wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) wakiwa na lengo la kuomba msamaha na kukiri kosa hilo.
Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, mwaka wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo 50 vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh milioni 392.8 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Pia inadaiwa Oktoba 26, mwaka huu, washitakiwa hao wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande vya meno ya tembo10 vyenye uzito wa kilo 13.85 vya thamani ya USD 30,000 sawa na Sh milioni 65.4.
Wanadaiwa kuwa Oktoba 27, mwaka huu, wakiwa Tabata Kisukuru washitakiwa hao walikutwa na vipande vinne vya meno hayo ya tembo yenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya USD 15,000 sawa na Sh milioni 32.7 .
Aidha, Oktoba 29, mwaka huu walikutwa na vipande 36 vya thamani ya Sh milioni 294.6 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...