Msanii wa kizazi kipya Khamisi Mwijuma ‘Mwana FA’ amepiga shoo moja matata ndani ya Tamasha la 38 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.
Katika onesho hilo, ukumbi huo wa TaSUBa ulifurika watu mbalimbali wadau wa burudani waliokuwa na hamu ya kumshuhudia msanii huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo ya ‘We endelea tu’.
Akiwa jukwaani pia alitumia wasaa huo kuwakumbuka wasanii waliotangulia mbele za haki akiwemo marehemu Mangwea na kumuelezea kuwa ni miongoni mwa wasanii waliokuwa na uwezo mkubwa sana na kumuenzi kwa kupiga wimbo wake wa "Mikasi".
Aidha, Mwanafa aliimba nyimbo zake kama "Asante kwa kuja", "Ya Laiti" na "Unanisikia".
Mwana FA aliwashukuru wadau hao kwa kupokea sanaa yake na kisha kuwaomba kuwaombea wasanii waliotangulia mbele za haki akiwemo Sharo milionea, Complex, King Majuto na wengine wengi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...