Na Khadija Khamis –Maelezo    Zanzibar              
Umoja wa Wakala wa Ajira Binafsi Zanzibar( ZAPEA ) umeishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapatia fursa ya kushiriki mkutano wa kimataifa nchini  Oman kwa lengo la kukuza ajira nchini .
Hayo yameelezwa na Kiongozi wa Msafara Amani Khamis Fakih (pichani juu) huko Uwanja wa Ndege wai Abeid Amani Karume wakati wakiondoka  kuelekea nchini Omani .
Amesema wataitumia vyema  fursa walioipata kwani wataweza kuondoa  changamoto wanazokumbana nazo  katika kazi zao kwa  vijana wanapokuwa nchini huko. 
Alieleza kuwa changamoto zinazojitokeza kwa baadhi ya vijana wanaokwenda kufanyakazi huko nchini Oman ni pamoja na kutofuata utaratibu wa ajira jambo ambalo husababisha migogoro na usumbufu wafanyakazi na waajiri wao.
Aidha alifahamisha kuwa Umoja wa Wakala wa Ajira Binafsi Zanzibar unapeleka wafanyakazi mbalimbali katika Serikali ya Oman kwa kuzingatia Sifa, Mkataba Sheria na vigezo ambavyo vinakubalika kisheria.
“Vijana  wanaopelekwa na Umoja wetu katika nchi tofauti kwa masuala mazima ya ajira tunahakikisha tunazingatia vingezo muhimu vinavyohitajika na kutiliana saini Mkataba na Kampuni  husika pamoja na kushirikiana na Serikali ya Zanzibar na Ubalozi”Alisema Amani 
Nae Bi Khadija Said amewataka vijana kutokata tamaa katika kutafuta ajira nje ya nchi kwani serikali inafursa nyingi kupitia kwa wawekezaji.
Mkutano huo wa Kimataifa ni wa Siku tatu unafanyika nchini Oman ambao  umetayarishwa kwa mashirikiano kati ya Serikali ya Oman na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...