Moureen Rogath, Kasulu

Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa  siku 15 Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT), na  mhandisi mshauri Fred Abel kutoka kampuni ya BICO na mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa chuo cha ualimu Kabanga wilaya ya Kasulu, mkoa wa Kigoma kupitia upya fedha Sh. Bilioni 10 za mradi huo baaada ya kutowiana na majengo ya chuo hicho.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa majengo ya  chuo hicho amesema mbali na kutoa siku hizo pia Profesa Ndalichako amesikitishwa na kasi ya ujenzi wa chuo hicho na kusema umekuwa ukisua sua na kwenda polepole na kwamba wamekwamisha wanafunzi wa chuo hicho kuhamia kwa wakati.

Profesa Ndalichako amesema pamoja  na maagizo hayo pia ametaka kupatiwa gharama za ujenzi za kila jengo katika chuo hicho, huku akidai  ujenzi wa  majengo ya chuo hicho hauendani na kiasi hicho cha fedha ambazo tayari wameomba kwa serikali. 

"Kama chuo hichi kingewahi kumalizika haraka nilitamani walimu waweze kuhamia kutokana na majengo ya chuo wanachosoma sasa yapo hatarini kuwadondokea , "amesema profesa Ndalichako.Akitoa taarifa kwa waziri Ndalichako , Kaimu Mkuu wa Kanda ya ujenzi Luteni Kanali Onesmo Njau amesema chuo hicho chenye majengo 10 , muda wa ujenzi ni miezi 15 na  mpaka sasa umefikia asilimia 25.

Mratibu wa mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu kutoka wizara hiyo Ignas Chonya  amesema anashindwa kuelewa kwanini ujenzi huo umekuwa ukienda taratibu wakati fedha za ujenzi huo zipo na zimeshapitishwa tayari na serikali.Waziri Ndalichako yupo mkoani Kigoma kukagua miradi mbalimbali ya elimu katika halmashauri ya Buhigwe na Kasulu, ambapo miradi hiyo inatokana na fedha za mradi wa lipa kwa matokeo(EP4R).


Waziri wa Elimu, Sayansi na Technolojia , ametembelea na kukagua miradi ya elimu katika shule ya sekondari Kigodya, Chuo cha ualimu Kabanga , shule ya sekondari Ruhita, Shule ya sekondari ya Nyantare ,Shule ya msingi Kasyenene, shule ya sekondari Kasangezi na chuo cha kilimo cha Bubondo wilayani Kasulu na kutoa maagizo.
Waziri wa Elimu, sayansi na teknolojia akikagua ujenzi wa chuo cha ualimu Kabanga kilichopo wilayani kasulu mkoani Kigoma kinachojengwa kwa fedha za serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...