Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
MKURUGENZI wa Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mwajuma Maguiza amesema pamoja na kuwepo kwa Sheria ya Haki ya Mtoto kwa miaka 30 sasa lakini bado takwimu za Jeshi la Polisi hapa nchini za mwaka 2018 zinaonesha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto kuongezeka kutoka matukio 13457 kwa 2017 hadi matukio 14419 kwa 2018 ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 6.6.
Ametaja baadhi ya vitendo vya ukatili ni ulawiti, ubakaji, mimba, ndoa za utotoni, vipigo na ukeketaji vitendo hivi vyote vinagandamiza haki za mtoto zilizosainiwa na Rais wa awamu ya pili wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi ambapo zilisainiwa ili kulinda haki za mtoto na kwamba utekelezaji wa Sheria ya mtoto (CRC), utekelezaji wake upo lakini hautiliwi mkazo ndio maana vitendo vya ukatili vinaongezeka mwaka hadi mwaka.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 31 mwaka 2019, Mkurugenzi huyo amesema kuwa kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili katika jamii na familia ndio imekuwa sababu kubwa. “Tumekuwa tukishuhudia watoto wakifanyiwa ukatili katika familia zetu, ukatili wa aina mbalimbali ikiwa wanaofanya ukatili huo kwa kiasi kikubwa wakiwa watu waliokaribu na mtoto kama familia, dugu, jamaa na rafiki”.
Hata hivyo utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa watoto kwa kipindi cha Desemba mwaka 2017 hadi Januari mwaka 2018 katika halmashauri 12 hapa nchini zinaonesha kuwa ilibaini uwepo wa watoto 6,393 wanaofanya kazi mitaani, kati ya hao wasichana ni 1528 na wavulana 4,865.
Pia utafiti huo ulibaini kuwa watoto 1,385 ilibaini wanaishi na kufanya kazi mitaani usiku hii ni kutokana na kutokuwajibika kwa familia katika kumudu majukumu yao ya kuwalea watoto, hivyo jamii inapaswa kuwajibika katika malezi ya watoto ili kujenga taifa lenye kutengemeana kuwepo na wazazi, watoto, vijana pamoja na wazee.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya watoto kutoka wizara ya Afya, Mwajuma Magiza akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wakitoa semina ya malezi ya watoto na msingi wa malezi ya watoto na familia
Frank Odhiambo akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa mafunzo ya malezi bora ya watoto na malezi bora ya watoto.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...