Na Woinde Shizza,Arusha.
SERIKALI imesema kuwa itahakikisha inaendelea kushirikiana na wawekezaji hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira mazuri ili waweze kufanya shughuli zao pasipo kuwa na bughudha zozote kwani wamekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa pato la Taifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo,Elisante ole Gabriel
aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika ziara yake ya
kutembelea kiwanda cha kusindika nyama cha Happy Sausage kilichopo
Sakina jijini hapa.
“Wawekezaji wamekuwa na mchango mkubwa sana katika kuinua pato la
taifa pamoja na uchumi wa n chi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na
kuchangia kupatikana kwa ajira nyingi kwa wananchi hivyo hawana budi
kuthaminiwa kwa mchango wao huo’’alisema Katibu Mkuu huyo.
Ole Gabriel alisema kuwa anatambua changamoto mbalimbali
zinazokikabili kiwanda hicho cha Happy Sausage ikiwemo mgogoro wa muda mrefu kati yake na halimashauri ya jiji la Arusha hali ambyo imekuwa
ikichangia kusuasua kwa uzalishaji na kuhahidi kulipatia ufumbuzi
ndani ya muda mchache.
Awali akimkaribisha Katibu Mkuu huyo,Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kiwanda hicho,Andrew Mollel alimweleza katibu mkuu huyo kuwa kiwanda hicho kilianzishwa mwaka 1990 na kwamba kimekuwa kikizalisha bidhaa zenye ubora ambapo kwa sasa kimejipanga kutanua soko lao kufikia nchi zote za Afrika Mashariki.
“Kiwanda kimeshindwa kufikia malengo ya kuongeza uzalishaji kutokana
na kujikuta ikikwamishwa kufanya ukarabati wa kiwanda hicho ilihali
serikali kupitia vizara ya mifugo na uvuvi kwa nyakati tofauti imekuwa
ikikitaka kiwanda hicho kufanya ukarabati imekuwa ndio changamoto yetu
kufikia malengo ya uzalishaji”.alisema Mollel
Mwenyekiti huyo wa bodi aliongeza kuwa pia halimashauri ya jiji la
Arusha imekuwa ikikwamisha ukuaji wa kiwanda hicho kwani imekataa
kutoa kibali cha ukarabati na upanuzi wa majengo ya kiwanda
hicho(building permit) jambo linalokwamisha uongezaji wa thamani na
uzalishaji hali ambayo imekuwa ni changamoto kubwa sana kwao na
kuiomba serikali kuu kuu kuingilia kati.
Mollel aliiomba Serikali kumpatia eneo lenye ukubwa wa ekari 300
katika eneo la Muriet jijini hapa ili aweze kuanzisha shamba kubwa la
mifugo litakalokiwezesha kiwanda hicho kufuga mifugo mingi ikiwemo
nguruwe kwani tayari wamekwishafanya mazungumzo na serikali ya
Ujerumani ambapo imewaahidi kuwapatia mbegu za nguruwe wanaokua kwa muda mfupi ukilinganisha na wa hapa Tanzania ambao huchukua muda
mrefu kukua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...