Na Woinde Shizza Michuzi blog,Arusha .
Watu 7 wakiwemo wenyeviti wawili wa vitongoji wametiwa mbarobi kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 520 katika eneo ka ujenzi wa moja kati ya visima 53 katika kata ya kikwe kijiji cha mawe wilaya ya Arumeru
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alisema kuwa kukamatwa kwa watu hao kumetokana na mtego alikuwa ameuweka mara baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa baadhi ya wananchi wanaoshirikiana na wafanyakazi na walinzi wanaolinda maeneo ya mradi kuiba vifaa vya ujenzi zikiwemo nondo , mabomba pamoja na mbao na mabati.
Alisema kuwa Kutokana na taarifa hizo ilimlazimu kufanya msako wa ghalfa na kustukiza katika nyumba za baadhi ya wananchina wafanyakazi wa mradi huo wanaodaiwa kuiba vifaa hivyo ambapo walifanikiwa kukuta nondo zaidi ya 40 zikiwa zimetelekezwa nje ya nyumba ya mwananchi mmoja ambae awali alikuwa akifanya kazi katika mradi huo baada ya wezi wa nondo hizo kustuka kuwa wanafuatiliwa na kuamua kukimbia
"msako huu ulianza alfajiri mpaka mchana na tumeamua kufanya zoezi hilo nanatoa onyo kwa watu wote wanaotaka kuhujumu miradi hii ya maji kuacha tabia hiyo mara moja nana sisitiza kuwa nitawachukulia hatua watu wote watakaobainika kuiba na kuficha vifaa vya ujenzi katika miradi"alisema Muro
Kwa upande wao baadhi ya watuhumiwa mbali na kukiri kuiba vitu katika miradi wamesema mtandao wa wizi huo ni mkubwa uku ukihusisha baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji ambavyo mradi huo unatekelezwa
Kwa upande wake Diwani wa kata ya kikwe Paul Shango ambae alikuwa kwenye kikosi cha mkuu wa wilaya cha kusaka wezi , mbali na alipongeza jitihada zinazofanywa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ya kusimamia miradi hiyo kikamilifu amewataka wananchi kutothubutu kuhujumu miradi hiyo kwa kuwa ina manufaa kwa wananchi haswa katika kuwapatia maji safi na salama
Katika hatua nyingi Mkuu wa wilaya ya Arumeru ametoa mwezi mmoja kwa kamanda wa polisi wa wilaya ya Arumeru mlowola kuwahamisha askari polisi ambao sio waaminifu wanaofanya kazi katika kituo cha polisi mbuguni kutokana na baadhi yao kutuhumiwa kuwalea wezi wanaoiba vifaa katika miradi hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiwahoji baadhi ya watuhumiwa wanaoabiliwa na tuhuma za wizi wa vifaa vya mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 520.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...