Klabu ya Taliss-IST imeshinda  ubingwa wa mashindano ya wazi ya kuogelea baada ya kukusanya pointi nyingi kushinda timu nyingine saba. Katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kisasa la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika(IST) Masaki, Klabu hiyo likusanya jumla ya pointi 2,207.

Klabu ya Bluefins chini ya kocha na muasisi  Rahim Alidina imeshinda nafasi ya pili kwa kupata pointi 1,281 wakati Klabu ya Morogoro, Mis Piranhas ilishika nafasi ya  tatu kwa kupata pointi 830. Klabu ya Dar es Salaam Swimming Club (DSC) ilimaliza katika nafasi ya nne kwa kupata pointi

750. Waogeleaji wa kike wa klabu hiyo walikusanya pointi  373  na wanaume walikusanya pointi 377.

Nafasi ya tano ilikwenda Mwanza ambao walipata pointi 468  huku FK Blue Marlins iliskinda nafasi ya sita kwa kupata pointi 429 na  Uwcea Moshi Kilimanjaro ikikusanya pointi 325 na Champion Rise katika nafasi ya nane kwa kupata pointi 244.

Meneja wa timu ya Taliss-IST, Hadija Shebe aliwapongeza waogeleaji wake kwa ushindi huo.

“Ushindi huu ni faraja kwetu na umetokana na juhudi na ushirikiano baina ya makocha, wazazi, wadau na waogeleaji kwa ujumla,” alisema Hadija.
Viongozi wa IST, TSA na waogeleaji wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi.
Mwenyekiti wa TSA, Imani Dominic akichumpa kuzindua bwawa la kisasa la kuogelea la IST.
Waogeleaji wakichumpa wakati wa mashindano ya Taifa ya kuogelea.
Mkurugenzi wa IST, Mark Hardeman akizungumza wakati wa uzinduzi.
Waogeleaji wakiwa katikapicha ya pamoja baada ya kushinda medali mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...