Na Woinde Shizza,Arusha
WANAUME hapa nchini wameshauriwa kuepukana na mfumo dume ambao kwa muda mrefu umekuwa ukiwakandamiza wanawake ikiwa ni pamoja na kuepukana na kuwadhania au kuwatumia wanawake kama kifaa cha kazi.
Hayo yalisemwa jana na Mwalimu Daniel Mgogo kutoka katika kanisa la Baptist la Tukuyu Mbeya,alipokuwa akizungumza katika kongamano la siku ya Mke Mwema,kongamano lililofanyika jijini hapa.
Alisema kuwa wakati umefika sasa kwa wanaume kubadilika na kuachana na dhana,desturi na mila potofu ambazo zimepitwa na wakati ambapo aliwasihi wadumishe upendo katika ndoa zao ikiwa ni pamoja na
kuwaheshimu wake zao.
“Mfumo dume unatakiwa upigwe vita na ukomeshwe,angalia mwanamke anabeba mimba kwa miezi tisa na mwanaume yupo tu,ila baada ya kujifungua motto ni wa baba,ni lini ulisikia mtoto kapewa jina la mama”alihoji .
Mwalimu Mgogo alisema kuwa wanawake hapa nchini wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo masuala ya mirathi kutokana na mfumo dume,ikiwa ni pamoja na kuachiwa peke yao jukumu la matunzo ya mtoto.
“Mwanamke anapoolewa anaamini kaolewa na mtu mmoja ila baada ya mudaanajikuta kaolewa na ukoo, wifi,shemeji,mama na baba mkwe kila mtu atakuwa anamtaka kufanya au kutofanya jambo Fulani na kila mmoja kwa wakati wake hali ambayo humfanya mwanamke asijue amsikilize nani na asimsikilize nani kwani muda mwingi huwa na hao,alisema
Naye Mhubiri kutoka huduma ya New Life in Christ ya Mkoani hapa,Mhandisi Tunzo Mnzava,ametoa wito kwa wanawake kuzingatia mafundisho kwani ndio msingi wa maisha ikiwamo kumtanguliza Mungu kwa kila jambo na kuhakikisha wanawaheshimu na kuwathamini waume zao.
Mhandisi Mnzava amewataka wawe waaminifu ikiwa ni pamoja na kuwa na utoshelezi kwa waume zao pamoja na kujiamini na watamani ndoa zao ziwe za milele,Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Mke Mwema,Aimbora Kwayu alisema kuwa kikindi hicho kilianzishwa mwaka 2011 na mpaka sasa kina wanachama zaidi ya 200 kutoka maeneo mbalimbali.
“Siku ya Mke Mwema huazimishwa tarehe kumi na nne oktoba kila mwaka ambapo huwakutanisha wanachama ambao wamegawanyika katika timu pamoja na wageni waalikwa mbalimbali lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano baina yao.
Alisema kuwa kikundi cha mke mwema kimegawanyika katika timu mbalimbali ambapo mpaka sasa wana timu tano ambazo ni Njiro,Moshono,Uswahilini,Wilayani na Sakina ambao ndio walioandaa
tukio hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...