Msimamizi wa miradi ya Tanzania Steel pipes Ltd Mhandisi Emmanuel Mwambapa akitoa maelekezo kwa Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maji Mhandisi Anton Sanga leo kuhusiana na namna wanavyotengeneza mabomba ya kupitishia maji taka na maji safi wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho ya makampuni zinazotengeneza mabomba ya maji safi na majitaka ,maonyesho yanayofanyika kwa muda wa siku tatu katika viwanja vya hotel ya Naura jijini hapa(picha na Woinde Shizza,Arusha).
Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya maji Mhandisi Anthony Sanga akifungua semina hiyo ya wahandisi wa maji
Mkurugenzi mwendeshaji wa taasisi ya wadau wa huduma za maji nchini (ATAWAS) Costantino Fidelis akifafanua jambo mbele ya wanahabari.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji ya plastiki (PLASCO LTD) Allimiya Osman akiongea na waandishi wa habari
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
Naibu katibu Mkuu wa wizara ya maji Mhandisi Anthony Sanga amezitaka mamlaka na wadau wa maji nchini kuhakikisha wanatumia ushirikiano na uzoefu wao kupata fedha na mikopo ya kujenga miradi ambayo itatoa huduma bora za maji kwa wananchi na kuacha tabia ya kuweka taarifa kwenye mafaili.
Sanga aliyasema hayo leo wakati akifungua warsha ya siku tatu ya wadau wa maji kutoka mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na shirikisho la wasambazaji wa maji nchini (Atawas) iliofanyika katika ukumbi wa hotel ya Naura Spring iliopo ndani ya halmashauri ya jijini Arusha.
Alifafanua kuwa thumuni la mafunzo haya ni kujadili namna ya upatikanaji wa fedha za miradi ya maji itakayowasaidia wananchi kupata huduma bora za maji safi na salama kwa bei nafuu kwa kuwatumia wadau wa taasisi za kifedha kupata mikopo ya ujenzi wa miradi midogo na mikubwa.
“Nawasihi washiriki wote muhakikishe mnaenda kutekeleza kwa vitendo yote uliofundishwa hapa ili wananchi wapate huduma bora za maji za bei nafuu sio kwenda na kuandika taarifa ziishie kwenye mafaili tunataka utekelezaji wenye tija kwa maendeleo ya tasnia ya maji nchini”alisisitiza Sanga.
Alieleza kuwa serikali ya awamu ya tano imejikita kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani hivyo kuwataka watendaji wote ndani ya wizara hiyo ziwemo mamlaka za maji mikoa kufanyakazi ya kutekeleza miradi kwa ubora kwa lengo la wananchi kupata huduma bora za maji ili kufanikisha azma hiyo ya serikali
Kwa upande wake mkurugenzi mwendeshaji wa taasisi ya wadau wa huduma za maji nchini (ATAWAS)Costantino Fidelis alisema kuwa uhaba wa maji unatokana na ukosefu wa fedha za ujenzi wa miradi ya maji ndio maana wameamua kuwajengea uwezo watendaji wa mamlaka za maji mikoa kupata mafunzo ya kuombea fedha za miradi kutoka kwenye taasisi za kifedha kutekeleza upatikanaji wa maji nchini
.
Alisema kuwa hayo ndio yamewafanya kuona umuhimu wa kuendesha warsha hiyo ili kuona miradi ya maji ikitekelezwa na kuondoa uhaba wa maji nchini ikiwemo kwenye suala zima la upatikanaji wa fedha kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani
Alibainisha kuwa kwanaamini mafunzo haya yatafungua milango kwa mamlaka za maji kuwa na fedha za kutosha kutekeleza miradi ya maji nchini ambayo itasaidia kuondoa uhaba wa maji kwa wananchi wengi zaidi hivyo kufikia malengo ya serikali
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji ya plastiki (PLASCO LTD)Allimiya Osman alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikizalisha mabomba ya maji yenye uwezo mkubwa duniani katika kuhimili, kuhifadhi na kupitisha maji kwa muda wa mrefu bila kuharibika.
Alisema teknolojia inayotumika kutengeneza mabomba hayo inatumika kote duniani hivyo kuwataka wadau wa maji nchini kuhakikisha wanashirikiana na wadau hao wa maji katika kukambiliana na changamoto za maji katika kuboresha huduma za maji nchini.
Alibainisha kuwa ili kufanikiasha suala zima la utoaji huduma wanasisitiza serikali na wadau wa maji kuangalia matumizi ya fedha wanazopata kwa kununua bidhaa za viwanda vya hapa nchini ili kuongeza wigo wa mapato na kupunguza tatizo la ajira.
Nae msimamizi wa miradi kutoka kiwanda cha kutengeneza mambomba cha Tanzania Steel Pipes Emmanuel Mwambapa aliomba serikali katika swala zima la manunuzi ,wanunue bidhaa zinazotengenezwa hapa nchi ili kusaidia kuingiza pato nchini.
"serikali tunaomba naomba mnavyowapa wakandarasi kazi muwasisitize wanunue bidha Za nyumbani ili tuweze kupata faida na kuingizia pato nchi,wakinunua bidhaa hapa nchi kazi zitaongezeka kwani uzalishaji utaongezeka na ukiongezeka tutaajiri watu zaidi kwaiyo ajira zitaongeza pia na pato la taifa litakuwa"alibainisha mwambapa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...