MFUMO wa One stop centre unaoendeshwa na jeshi la polisi umeisaidia jamii ya watanzania hususani wakazi wa Ilala katika uwasilishaji wa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na kamishna msaidizi wa polisi Zuberi Chembera wakati wa kongamano la siku 16 dhidi ya ukatili wa kijinsia uliofanyika kwenye viwanja vya kampala vilivyopo katika maeneo ya Gongo la mboto.

Amesema kutokana na uanzishwaji wa kituo hicho kumekuwa na uelewa kwa wananchi katika ufatiliaji pamoja na utoaji wa taarifa za matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia unaofanywa na baadhi ya watu ndani ya jamii.

"Matukio ya kikatili dhidi ya wanawake na watoto yamekuwa yakiongezeka kwa kadiri miji inavyopanuka na makazi kuongezeka ambapo baadhi ya wanajamii zikiwemo familia huishi kwa kuwekeana chuki, fitina ,wivu na imani mbalimbali za kidini," alisema Chembera

Chembera amesema kuwa jeshi la polisi limekuwa bega kwa bega na kikosi cha ulinzi shirikishi sambamba na wananchi katika kuhakikisha taarifa za matukio ya ukatili zinazowafikia zinachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi  na wadau mbalimbali wameanzisha madawati ya kijinsia yapatayo 25 kimkoa katika kuwezesha taarifa kufika kwa haraka.

Aidha takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2018 matukio ya makosa ya ubakaji yalikuwa 926 ambapo mwaka 2019 yalifikia 725,huku makosa ya ulawiti kwa watoto yakiwa idadi ya 471 kwa mwaka 2018 na kuongezeka kwa idadi ya 571 mwaka 2019, upewaji ujauzito Watoto wa kike mwaka 2018 ilikuwa 54 ambapo mwaka 2019 kupungua kwa idadi ya 51.

Kwa upande wake diwani wa gongo la mboto Jackob Kissi alisema kuwa matendo ya unyanyasaji wa kijinsia yameongezeka kutokana na malezi mabaya ya baadhi ya familia.

Amesema changamoto za kijinsia dhidi ya watoto na wanawake vinachangiwa na mfumo dume kuchukua nafasi kutenda ama kufanya matendo mabaya ndani ya  familia hizo.

Naye kamishna msaidizi wa polisi mnadhimu namba moja katika mkoa wa kipolisi Ilala Janeth Stephano alisema wananchi washiriki kikamilifu katika utoaji wa taarifa hivyo wasiwaogope polisi katika kuwalipoti wahusika waovu.
Kamishina msaidizi wa polisi Zuberi Chembera ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye  kongamano la siku 16 za kuadhimisha ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...