Mkuu wa Wilaya  ya Tandahimba  Sebastian Waryuba  amesema kiasi Cha shilingi Milioni 20 na mabati 300 ambazo zilitolewa kwa shule 107  za Kampeni ya shule ni choo zamewaafikia walengwa.

Akitoa tathimini  ya ziara yake katika shule hizo alisema kuwa hamasa katika vijiji kuhusu Kampeni hiyo ni kubwa

"Nimezifikia shule zote ambazo Kampeni hii inafanyika  tumewaongezea nguvu  kwa kuwapatia fedha  taslimu na mabati,"alisema Waryuba

Fedha  hizo zimetolewa na RC wa Mtwara Gelasius Byakanwa katika Kampeni yake ya Shule ni choo yenye lengo la kuondoa tatizo la matundu ya Choo kwa shule za Msingi na Sekondari .
 Wananchi waliendelea na ujenzi wa matundu ya vyoo

 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akikabidhi shilingi Milioni moja kwa mwalimu Mkuu wa Mivanga
 Ofisa Maendeleo ya Jamii Aloyce Masau akisaidia kuwashushia zege mafundi
 DC Waryuba akiwa na afisa Mipango Kassim Lihumbo wakisaidia kazi katika Kampeni ya shule ni choo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...