Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Wakala wa Meli Nchni (TASAC) imesema kuwa katika kufanya kazi zake wale waliokuwa mawakala Forodha wasiokuwa waaminifu wataondoka wenyewe katika kufanya biashara hiyo.

Akizungumza jana Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Dkt. Emmanuel Ndomba amesema TASAC haiko tayari kuona watu wakitapeliwa akifafanua kuwa usafirishaji kwanjia ya bandari itumike kama kichocheo cha kuiingizia serikali mapato.

Moja ya majukumu yake kwa sheria ni utekelezaji wa uhakiki wa mizigo zinazoingia bandarini pamoja na uwakala wa meli za mafuta , kijeshi,utalii pamoja na meli za utafiti wa mafuta baharini.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema wameingia kwenye kazi za forodha za meli,si kwaajili ya kuziondoa taasisi binafsi zinazofanya kazi za meli tunachokwenda kufanya, ni kutumia nguvu yetu ya serikali kurudisha kila mteja ambaye yupo katika nchi tulizopakana nazo ambao awali walikuwa wakitumia huduma zetu na wakaacha,

“Mawakala binafsi wa forodha tunawahakikishia kuwa kuingia kwetu kwenye kazi hii si kuwanyanganya kazi bali ni kuwafaidisha,tahadhari wawe waaminifu katika kufanya biashara ile kama watakuwa na tabia ya kuwadhulumu wananchi waache mara moja kwasababu hii itawatoa katika biashara hatutorusu tapeli kuendelea na biashara”amesema.

Amesema utendaji wa TASAC umejikita katika maeneo manne ambayo ni uwakala wa meli,uhakiki wa mizingo na udhibiti wa nyaraka ambapo kuanza kwa shughuli hizo ni utekelezaji uwakala huo.

“ Tunafanya kazi kulingana na sheria kuna watu wamekuwa wakilalamika kwamba tozo zetu ni kubwa lakini sisi tunazingatia taratibu za kisheria ili kupata tuzo inayostahili kwa mujibu wa sharia pamjoa na kupunguza utitiri wa tozo saba zilizokuwepo zilizokuwa zikiwanyanyasa wananchi na tukazifuta kupitia sheria iliyoanzisha shirika ”alisema. Nae Mkurugenzi Udhibiti wa Majini na Bandari Deogratius Mukassa amesema kwa mawakala binafsi wa forodha watakaokuwa wakifanya kazi kwa uaminifu watakuwa na uhakikia wa kazi huku wezi akisema ndio kiama chao.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Meli Nchini (TASAC ) Dkt. Emmanuel Ndomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utendaji wa wakala huo namna wanavtokwenda katika kuhakikisha nchi inapata maendeleo kutokana na meli zinazoingia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...