Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto), akizungumza na
Watumishi wa Wizara yake, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo,
jijini Dodoma, leo. Kingu amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya
kazi kwa ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020. Aliyevaa
tai ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima.

Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto), akizungumza na
Watumishi wa Wizara yake, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini
Dodoma, leo. Kingu amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa
ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020. Katikati ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima, na kushoto ni Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimaliwatu, Emmanuel Kayuni.

Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto), akimsikiliza
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara hiyo, Emmanuel Kayuni,
alipokuwa akifafanua jambo katika kikao cha Watumishi kilichofanyika,
katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Meja Jenerali
Kingu amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na
kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Ramadhan Kailima.

Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (katikati), akizungumza na
Watumishi wa Wizara yake, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo,
jijini Dodoma, leo. Kingu amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya
kazi kwa ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020.

Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (katikati), akizungumza na
Watumishi wa Wizara yake, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo,
jijini Dodoma, leo. Kingu amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya
kazi kwa ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa 2020. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………..
Na Mwandishi Wetu, MOHA, Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amewataka Watumishi wa Wizara
yake kufanya kazi kwa ushirikiano na kujituma zaidi kwa mwaka mpya wa
2020.
Meja Jenerali Kingu ameyazungumza
hayo katika kikao na watumishi wa Wizara hiyo, kilichofanyika ukumbi wa
mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo, ambacho kikao hicho kililenga
kutoa salamu za mwaka mpya wa 2020 na kuwataka kuendelea kufanya kazi
kwa kasi ndani ya mwaka huu.
“Lengo la kikao kikao hiki ni
kupeana salamu za mwaka mpya, na pia tunapaswa kumshukuru Mungu kwa
kutufikisha mwaka huu salama, wengi hawakufika lakini mimi na wewe
tumefika, hivyo tuendelea kufanya kazi kwa upendo,” alisema Kingu.
Aliongeza kuwa, Mwaka 2020 ni
mwaka wa kazi na ushirikiano, licha ya kuendelea kufanya majukumu yetu
lakini watumishi wawe wazi katika masuala yote ya kazi ili kuleta
ufanisi na mafaniko ndani ya Wizara hiyo.
“Mwaka huu tunapaswa tubadilike
zaidi, tufanye kazi, kila mtu awajibike kutokana na kazi anazozifanya,
Mungu atupe uzima na afya, tuwe na umoja, upendo katika kutekeleza
wajibu wetu kisawasawa, na atakayefanya kazi atapewa haki yake na siyo
kuishi kiujanjaujanja,” alisema Kingu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimaliwatu (DAHRM), Emmanuel Kayuni, alimshukuru Katibu
Mkuu kwa kikao hicho, na kuwataka watumishi kufuata maagizo yake na pia
kuendelea kufanya kazi kwa umoja na kutii sheria za kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...