Charles James, Michuzi TV
TAASISI za Umma nchini zimetakiwa kuwajibika kuhakikisha zinaendana na azma ya Serikali kwa kuboresha mifumo ya kielekroniki inayoandaa Ankara ili iweze kuwarahisishia walipaji wa huduma za serikali kupata ankara zao kwa urahisi na haraka.
Pia wametakiwa kutekeleza matakwa ya waraka namba tano wa Hazina unazozitaka taasisi zote kuhakikisha zinapata ridhaa ya Wizara ya Fedha na Mpango na Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) kabla ya kufanya ununuzi, uandaaji, usimikaji na utumiaji wa mfumo wowote wa kielektroniki wa usimamizi wa fedha za umma.
Maagizo hayo yametolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mpango, Dotto James wakati alipokua akifunga mkutano wa mwaka wa watumiaji wa mfumo wa serikali wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato (GePG).
Amesema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mpango kuhakikisha mfumo wa GePG unaleta tija katika ukusanyaji wa fedha za umma bado baadhi ya taasisi za umma hazijaboresha mifumo yao ya kuandaa ankara.
" Kwa kufanya hivyo serikali itaweza kukusanya fedha kwa wakati na kutoa huduma bora kwa umma hivyo ili kujihakikishia kuwa mfumo wako unafuata viwango stahiki katika kuandaa taarifa za ankara hakikisha unawasiliana na idara ya usimamizi wa mifumo ya kifedha ili uweze kupatiwa muongozo," Amesema James.
Katibu Mkuu pia amezitaka taasisi ambazo hazijaandaa mifumo yao kuhakikisha inaandaa ndani ya muda unaotakiwa tofauti na hapo wote wanaohusika watawajibika lakini pia amewaagize wataalamu wa Idara hiyo kujitahidi kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa kufanya miamala hii ili kuwapa unafuu wananchi.
Amesema wanazindua mfumo huo wa GePG toleo la simu za mikononi (GePG App) ili kuongeza ufanisi na urahisi katika kulipia huduma za umma huku pia akiahidi kuhakikisha wanawapa elimu ya kutosha watu wanaowahudumia ili kuendana na mfumo huo.
" Mfumo huu umetusaidia sana katika ukusanyaji wa mapato, mambo yote yapo hadharani siyo gizani tena. Kupitia mfumo huu hata Mhe Rais anaweza kuona makusanyo ya Halmashauri na Taasisi zote za serikali kila ndani ya dakika moja, niwapongeze sana kwa kuandaa mfumo huu," Amesema James.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mifumo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw John Sausi amemshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Fedha kwa namna ambavyo amekua msaada kwao katika kuhakikisha wanafanikisha malengo yao ya kukamilisha mfumo huo.
Amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto kwa baadhi ya watumiaji ambazo wameshaanza kuzitatua mfumo huu ni rafiki katika kulipia Bill zote na kutoa wito kwa taasisi za Kibenki na makampuni ya Simu kuchukua maoni kwa wateja wao ili kuweza kushughulikia changamoto watakazozibainisha.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James (mwenye suti nyeusi) akizindua mfumo wa serikali wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato (GePG) leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mifumo kutoka Wizara hiyo, John Sausi na Mwakilishi wa Mabenki, Domino Tarimo.
Mwakilishi
wa Mabenki, Bi Domina Tarimo akielezea namna ambavyo wamekua
wakinufaika na mfumo wa GePG wakati wa mkutano wa watumiaji wa mfumo huo
leo jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James akizungumza na watumishi
kutoka Wizara ya Fedha, Taasisi za Simu na Mabenki pamoja na wandishi wa
habari jijini Dodoma leo wakati wa kufunga mkutano wa watumiaji wa
mfumo wa serikali wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw Dotto James akizungumza katika
mkutano wa mwaka wa watumiaji wa mfumo wa serikali wa kielektroniki wa
ukusanyaji wa mapato GePG jijini Dodoma leo.
Mkurugenzi
wa Mifumo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, John Sausi akielezea namna
ambavyo mfumo wa serikali wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato
(GEPG)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...