SHULE ya St. Anne Marie Academy imefanikiwa kuwa ya kwanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika matokeo ya darasa la nne huku wanafunzi wake tisa wakiingia 10 bora kitaifa kwa wasichana na wavulana.

Kwenye matokeo hayo yaliyotangazwa na Baraza la taifa la Mitihani (NECTA), shule hiyo imefanikiwa pia kuwa ya kwanza kwa Wilaya ya Ubungo na kuwa ya tisa kitaifa.

Akizungumzia matokeo hayo Mkuu wa shule hiyo iliyoko Mbezi kwa Msuguri, Gladius Ndyetabura, amesema kuwa kwenye matokeo hayo, wanafunzi wote waliofanya mtihani wa darasa la nne walipata wastani wa alama A.

Amesema hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyepata darala B, C, D wala E na mbali na hilo wanafunzi wao tisa wamefanikiwa kuingia 10 bora kitaifa na kwamba wanawashukuru walimu kwa mafanikio hayo.

"Maana kuwa na wanafunzi 130 na wote kupata daraja A na kuingiza tisa katika 10 bora si kazi rahisi. Wanafunzi wa shule hiyo walioigia 10 bora kwa wavulana ni Elisha Mphuru aliyeshika nafasi ya pili kitaifa, Juma Bufe nafasi ya tatu kitaifa na Abdalah Lipagila nafasi ya saba kitaifa.

'Wasichana wa shule yetu walioingia 10 bora kuwa ni Bernice Mwakalinga ambaye ameshika nafasi ya sita kitaifa, Dorine Komba nafasi ya saba na Zanula Mpandula ambaye ameshika nafasi ya nane,amesema.

Kwa upande wa kidato cha nne, amesema wanafunzi 43 wamepata daraja la I, wanafunzi 63 daraja la II, wanafunzi 19 daraja la III na wanafunzi sita daraja la nne.Kuhusu matokeo ya kidato cha pili, Ndyetabura amesema wanafunzi 49 walipata daraja la I, wanafunzi 22 daraja la II, wanafunzi 23 daraja la tatu na wanafunzi saba daraja la nne.

Ametaja siri ya mafanikio ya shule yake kuwa ni kufundisha kwa bidii na kufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi wake na kwamba mwaka huu wanatarajia kufanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya darasa la saba.

“Kusimamia nidhamu ya wanafunzi na kushirikiana na wazazi ni moja ya siri ya mafanikio ya shule hii na pongezi tulizopata ni motisha kwamba tunatarajia kufanya vizuri zaidi ya hapa,” amesema
Ndyetabura amesema kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2018, St Anne Marie ilikuwa ya kwanza kwa Wilaya ya Ubungo, ya kwanza kwa Mkoa wa Dar es Salaaam na ya sita kwenye ngazi ya kitaifa.

“Tumekuwa tukifanya vizuri mwaka hadi mwaka kwenye matokeo ya wilaya, mkoa na kitaifa na kutokana na maandalizi mazuri tuliyoyafanya kwa wanafunzi wetu mwaka huu tunatarajia kufanya vizuri sana kwenye matokeo ya darasa la saba,” ameongeza.

Amewashukuru wazazi wa wanafunzi kuwa wamekuwa chachu ya ushindi wa shule hiyo kutokana na ushirikiano wanaotoa kwa uongozi wa shule hiyo kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.Ndyetabura amewashukuru pia walimu wa shule hiyo kwa namna wanavyojituma usiku na mchana kuhakikisha wanafunzi wanaofanya mtihani wanapata alama za juu.

“Shukrani za kipekee ziwaendee walimu wangu kwasababu hawapumziki wanafanyakazi usiku na mchana, Mkurugenzi wa shule Jasson Rweikiza naye amekuwa nguzo kubwa kwenye ushindi huu kwa namna anavyotupa kila aina ya ushirikiano tunampongeza sana,” amesema.


   Mkuu wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi kwa Msuguri, Gladius Ndyetabura akiwapa zawadi ya fedha wanafunzi 9 wa shule hiyo walioingia 10 bora kitaifa kwenye matokeo  ya darasa la nne na kuiwezesha shule hiyo kuwa ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya ya Ubungo kwenye matokeo hayo.
Mkuu wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi kwa Msuguri, Gladius Ndyetabura akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo aliyeingia 10 bora kwenye matokeo ya darasa la nne mwaka huu na wenzake nane na kuiwezesha shule hiyo kuwa ya kwanza mkoa wa Dar es Salaam, Ubungo na ya tisa kitaifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...