Raia  30 wa hapa waliorudishwa wakiwa katika kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili wakitokea Afrika Kusini.

Raia  30 wa hapa nchini waliorudishwa,wakitokea Afrika ya Kusini wakiwa katika mahaka ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili hapa nchini.

Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

RAIA  30 wa Tanzania waliorudishwa nchini wakitokea Afrika ya Kusini ambako walikuwa wanaishi kinyemelea kwa muda usiojulikana wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za kusafiri nje ya nchi kinyume na sheria.

Kati ya hao, washtakiwa 16 wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa serikali kutoka Idara ya Uhamiaji ni Godfrey  Ngwijo mbele ya hakimu mkazi Mwandamizi Augustine Mmbando ambapo wanadaiwa Januari 21, 2020 huko katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wakiwa raia wa Tanzania walikutwa wakiwa wametoka nje ya nchi bila kufuata utaratibu wa Uhamiaji wa  kutoka nchini kwenda Afrika Kusini kwa kupitia mipaka inayojulikana.

Washitakiwa wote walikubali mashitaka hayo na upande wa mashitaka uliwasomea maelezo ya awali ambapo amedai tarehe zisizofahamika walitoka Tanzania na kuingia Afrika Kusini bila kufuata taratibu.

Ngwijo alidai katika tarehe hiyo, washitakiwa walikamatwa nchini Afrika Kusini na kuletwa Tanzania na kwamba walifikishwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kwamba walipelekwa Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuchukuliwa maelezo.

Washtakiwa hao wamehukumiwa kutumikia kifungo cha  miezi sita gerezani ama kulipa faini ya sh laki tatu kila mmoja. Ambapo baadhi yao wamefanikiwa kulipa faini na wamechukuliwa na wazazi wao.

Washitakiwa hao ni Omary Kaulu, Dominic Fabric, Sefu Mohammed, Hamad Hashiri, Asbawi Omar, Abdala Hamad, Razan Ally, Moosa Salimu, Mawki Ally, Daniel Joshua, Amari Abduli, Abdullah Ramadhan, Mohammed Tuwa, Aziz Mohammed, Rajabu Shabani na Adam Seifu.

Hata hivyo, washitakiwa hao kwa nyakati tofauti waliomba mahakama iwapunguzie adhabu kwa sababu wamekaa sana gerezani walipokuwa Afrika Kusini, wameikosea serikali ya Tanzania pamoja na serikali waliyotoka hivyo wapewe onyo na kupunguziwa adhabu.

Awali, akisoma mashitaka Ngwijo  alidai washitakiwa hao walitoka nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume  na kanuni za uhamiaji namba 20 (3) (a)  G.N namba 657 ya mwaka 1997 inayosomwa pamoja na kifungu namba 48 (2) ya Sheria ya Uhamiaji namba 54 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.

Washtakiwa wengine ni Adam Luzz, Suleiman Saidi, Kapaya Fredric, Semboko Abubakari, Mambosasa Francis, Juma Muhina, Chale Othoman, Salehe Iddy, Mohammed Kassim, Hassan Ally, Boban Abed, Abdul Kessy, John Joseph na Mawazo Frank ambao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally.

Hata hivyo, washtakiwa hao wamehukumiwa kulipa faini ya sh.50,000 ana kwenda jela miezi 18.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...