Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mawasiliano na Habari kwa Umma kutoka Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ( RSA) Ally Nurdin
Na.Vero Ignatus,Pwani.
Taasisi ya Mabalozi wa usalama barabarani
(RSA)kwa kushirikiana na wadau
wengine wameiomba serikali kuangalia upya sheria ya usalama barabarani nchini
Tanzania iliyotungwa mwaka 1973 ambapo sheria hiyo imerithi kanuni mbalimbali
zilizotungwa tangia mwaka 1933 ambapo zimeendelea kuboreswa kipindi hadi
kipindi.
Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi wa
Idara ya Elimu Mawasiliano na Habari kwa Umma( RSA) Ally Nurdin amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2018
marekebisho makubwa ya sheria hiyo ya usalama barabarani sura ya 168 ni yale
ambayo yalifanyika mwaka 1996.
''Marekebisho hayo yalifuata baada ya
hapo yalihusu ongezeko la faini tu bila kugusa vipengele vya msingi vya sheria
yenyewe kwasababu tangu wakati huo hadi sasa idadi ya magari inaongezeka
barabarani idadi ya watumiaji wa vyombo vya moto inaongezeka pamoja na vyombo
tofautitofauti ambavyo havikuwepo wakati huo pia vinatumika barabarani na tabia
za watumiaji wa vyombo hivyo zinabadilika kwa kuongezeka tabia nyingi mpya
ambazo hazikuwepo''Alisema
Nurdin alimesema kuwa vipengele vinavyotakiwa
kufanyiwa marekebisho ni pamoja na kifungu cha 5 kuhusu usajili wa magari
lakini hakiweki wazi iwapo usajili huo ni ule wa kieletroniki ili mmiliki wa
gari asilazimike kutembea na gari muda wote,kwasababu kadi inaweza kuwepo mkwenye
simu au kwenye App fulani,ambapo sheria ni wakati wake kutambua jambo hilo.
Amesema kuhusu umri wa kumiliki gari
kifungu cha 10(20)sheria ilivyo sasa inamapungufu inampiga marufuku mtu aliye
chini ya miaka 18 kumiliki gari hata hivyo aliye na miaka 14 anaruhusiwa
kumiliki pikipiki,amesema yapo maoni kwamba sheria hiyo isiruhusu kabisa aliye
chini ya miaka 18 asimiliki pikipiki wala gari japo kuwa maoni mengine
yanakinzana na kusema aruhusiwe.
''Swali linakuja je mmiliki akitaka kuuza
atauzaje wakati kuna mikataba inayosema kuwa aliyechini ya miaka 18 haruhusiwi
kui ngia katika mkataba,wakati huo huo ikitokea kwamba kuna makosa yanamhusu
mmiliki wa gari kushtakiwa au kufungwa au kulipa faini je atalipaje kwa mmiliki
wa umri wa chini ya miaka 18?'' Aliuliza
Aidha amesema kuwa katika faini kutumia
gari bila kusajili sheria hiyo katika kifungu cha 8(2) ambapo faini yake ni
shilingi elfu hamsini tu au kifungo kisichopungua miaka mitano,amesema faini
hiyo italipwa mahakamani iwapo mtuhumiwa atakutwa na hatia,jambo ambalo
barabrani faini yake ni shilingi elfu thelathini.
Amesema kuwa kifungu cha 11(4)kuharibu au
kubadili alama za utambulisho wa gari inamtaka alipe faini ya shilingi elfu
kumi ambapo adhabu hiyo ni ndogo kwa wanaofanya makusudi ili wasitambulike
wanapofanya makosa,amesema kifungu cha 14(5) kosa la kutoweka au kuficha alama
ama kuongeza alama za utambulisho wa gari adhabu yake ni shilingi elfu tano
ambapo haimfanyi mhusika kuijutia kosa.
Aidha Amesema kifungu cha 18 kinahusu
kosa la kutumia gari bila alama za utambulisho au kutumia alama za utambulisho
wa gari lingine au kutoa taarifa za uongo kuhusu usajili wa gari ambapo kosa
hilo kwa sasa adhabu yake shilingi 10,000 Kwani makosa ya makusudi kama haya
adhabu yake ni ndogo,kifungu cha 19 kosa la kuendesha gari pasipokuwa na leseni halali au kumruhusu asiye na leseni adhabu ya kosa hilo nayo ni shilingi 10,000
Ameainisha kuwa kifungu cha 21(1) leseni ya lena kwa dereva mwanafunzi wa udereva wa pikipiki amesema sheria iliyop[o sasa haimlazimishi anayejifunza kukata leseni ya lena kabla ya kuanza kujifunza kuendesha hivyo ni vyema seria ikaweka hitaji hilo kwa madereva wa pikipiki na bajaji,kifungu cha 23(7)kinachompa mamlaka mtahini wa udereva kumpitisha dereva kwa amefaulu na hivyo anafaa kupewa leseni na msajili.
''Kifungu hiki hakimwajibishi afisa yeyote wa serikali au mtahini au mtu yeyote aliyejiusisha katika kufanya udanganyifu wa kumtafutia mtu leseni ya usereva ambaye hana sifa za zinazostahili,hivyo sheria na kanuni haziweki bayana sifa ambazo anatakiwa mtahini kuwa nazo huyo anayetakiwa kutahini madereva wanafunzi ,hivyo ifike wakati sasa sheria ikafanyiwa marekebisho ili kuweza kuwaadhibu Maofisa kama hawa''alisema.
Kwa upande ambao unamruhusu sajili kumpa
mtu leseni ya udereva kwa kutumia uzoefu wake bila kupitia shule kifungu hiki
kwasasa yafaa kirekebishwe kwa kumtaka kila mtu kupita katika shule ya udereva
uliyo sajiliwa rasmi kwa ajili ya kufundisha madereva kabla ya kupata leseni.
kwa upande wake mkurugezi msaidizi wa habari
na mawasiliano kwa umma kutoka taasisi ya mabalozi wa usalama barabarani (RSA )Ramadhani
Msangi aliainisha baadhi ya orodha ya makosa yanayoweza kumfanya mtu
afungiwe leseni yake au kufutiwa na (mahakama lazima ifungie au kufuta
leseni)kifungu cha 27(1)kinatoa orodaha ya makosa amabayo kwayo leseni inaweza
kufungiwa au kufutwa kwa lazima ya mahakama
Amesema kuwa makosa lazima ambayo yanaweza
kufutwa leseni kwa muda wa miaka mitatu kwa mujibu wa kifungu cha cha
sheria 27(1) dereva anaweza kufutiwa leseni na mahakama,iwapo kwa mara ya
kwanza ametenda makosa kama vile
kusababisa madhara ya mwili au kifo kwa njia ya uendeshaji wa hatari,kutokuwa
makini barabarani,kuendesha kwa papara au kwa hatari,kuendesha gari dereva huku
akiwa amekunywa pombe au ametumia madawa ya kulevya,kuendesha akiwa hana leseni
halali au wakati leseni ikiwa imefutwa au kufungiwa
''Dereva anaweza kufungiwa au kufutiwa
leseni iwapo atakuwa ametenda makosa ya hatari kwa mara ya kwanza kutokuwa
makini barabarani,matumizi mabaya ya gari lake barabarani bila kujali watumiaji
wengine wa barabara ,kutokuifanya hai leseni yake na kuondolewa sifa za
kuendesha gari''Alisema
Aidha ameyataja makosa mengine kuwa ni
sambamba na dereva kufungiwa leseni kwa muda wa miezi sita iwapo kwa
mara ya pili ametenda makosa yaleyele ya awali,kufungiwa kuendesha gari kwa
muda wamiezi 12 iwapo atakuwa hajatimiza wajibu wake baada ya ajali mfano
kusaidia majeruhi wakati ilikuwa salama kufanya hivyo au kutoripoti ajali kwa
wakati,
Pia dereva anaweza kufungiwa leseni
kutokana na ulevi iwapo atakuwa na kiwanmgo cha ulevi kisichozidi 150mg
katika 100mls za damu atafungiwa kuendesha kwa miezi sita na endapo atarudia
atafungiwa kwa miaka mitatu,kilevi kilichozidi 150mg atafungiwa kuendesha kwa
miaka miwili na endapo atarudia atafungiwa kwa miaka sita.
Amesema mapendekezo katika sehemu hii ni
kuondoa kosa la kifungu cha 40:kusababisha madhara kwa mwili au kifo kupitia
uendeshaji wa hatari linalojitokeza katika kifungu kidofo cha kwanza cha aya ya
a-d ya kifungu cha 27(1)madereva hatari wapewe adhabu kali zaidi wakati
wale madereva wazembe wapewe adhabu ya chini kidogo
Aidha inapendekezwa kipengele h kuhusu
makosa ya ulevi katika kifungu cha 27(1)kifutwe chote ili adhabu zake
zibakie katika kifungu cha 44-49 ambapo kinahusu nmakosa yanayohusiana
na ulevi,pia wameshuri katika sehemu hiyo yachambuliwe vizuri ili wanaoendesha
kwa hatari barabarani bila kujali watu wengine leseni zao zifunguiwe kwa muda
mrefu zaidi na katika kipindi ambapo leseni zao
zifungiwe walazimishwe kurudi shule.
Amehitimisha kwa kusema kuwa wanahitaji
marekebisho ya sheria ya usalama barabarani kwa kuyapa kipaumbele yanatakiwa ya
haraka ni yale ya yanayohusu ulevi,mwendokasi,ufungaji wa mikanda,uvaaji wa
kofia ngumu (helmeti) magari madogo,amesema hayo ndiyo mambo ambayo RSA wa
kuchagiza marekebisho ya sheria ya usalama barabarani imeyalenga kwa sasa .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...