Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa akifungua mafunzo ya siku moja kuhusu kuzuia na kupambana na rushwa  kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mafunzo hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa  Serikali na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU).
 Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma kutoka TAKUKURU Bw. Joseph Mwaisalo ndiye aliyekuwa mwezeshaji wa mafunzo hayo akiwa amefuatana na  Bi. Stella Mpanju. Bw. Mwaisalo amesisitiza kwamba rushwa ni zaidi ya hongo na kuwataka watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kujiepusha na vitendo vya rushwa kutoka na unyeti wa Ofisi hiyo.
Washiriki wa Mafunzo hayo walikuwa ni Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Wakuu wa Vitengo, Mawakili wa Serikali na  Watumishi wa Kada mbalimbali.

Imeelezwa kwamba, Ukiukwaji wa maadili, upendeleo,  ubinywaji wa maslahi ya watumishi  na watumishi  kutopewa nafasi ya  kutoa mawazo yao, ni baadhi ya mambo yanayoweza kupelekea uwapo wa vitendo  vya kutoa na kupokea rushwa sehemu ya kazi.
Hayo yameelezwa leo (Ijumaa) na Mkurugenzi wa  Elimu kwa  Umma kutoka Taasisi ya Kuzuia na   Kupambana na Rush(TAKUKURU) Bw. Joseph Mwaisalo, wakati alipokuwa akitoa  mafunzo kuhusu uzuiaji na kupambana na rushwa kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mafunzo hayo na ambayo yalifunguliwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DkT. Evaristo Longopa,yamewahusisha watumishi wote kuanzia  Wakurugenzi wa  Idara,  Wakurugenzi Wasaidizi, Wakuu wa Vitengo, Mawakili wa Serikali na watumishi wa Kada Mbalimbali waliopo  Jijini Dodoma.
“ Rushwa ni zaidi ya hogo”. Anasema Bw. Joseph Mwaisalo. Na kuongeza. “Rushwa ni mmomonyoko wa maadili, mtumishi anaponyimwa haki yake ya kupandishwa cheo, au stahili yoyote ile ambao ni haki yake inatengeneza  mazingira ya rushwa.
Na kwa sababu hiyo, amewataka watumishi wa  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali siyo tu kuhakikisha wanazuia uwepo wa mianya  ya utoaji  na  upokeji wa rushwa lakini ni vizuri kwao pia kuzitambua haki zao, kuzidai kwa misingi ya sheria, taratibu na kanuni na kwa Menejimenti kuhakikisha kwamba inazingatia maslahi ya watumishi wake.
Akasema, watumishi wengi na hata wananchi waliowengi hawazijui haki zao na namna halali ya kuzidai haki zao na ndio maana wengi wao wanaishia kuombwa rushwa ikiwamo rushwa ya ngono.
“Rushwa ipo kila mahali, hata hapa katika Ofisi ya Mwanasheria kunauwezekano wa kuwapo kwa mazingira ya rushwa  kupitia utekelezaji wa majukumu yenu hasa mkizingatia  kwamba hii ni Taasisi  nyeti sana na ambayo ni mdau wetu mkubwa katika mapambano dhidi ya rushwa”. Anasisitiza Mkurugenzi wa  Elimu kwa Umma.
Akasema kutokana na unyeti wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na umuhimu wake kwa Taifa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jeneral John J. Mbungo, ameguswa sana na uamuzi wa Taasisi  hii muhimu wa kuwa na mafunzo haya ya kuelimishna juu ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa watumishi wake.
Bw. Mwaisalo ameitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakikisha kwamba, katika utekelezaji wa  majukumu  yake yakiwamo ya  upekuzi wa mikataba, uandishi wa sheria, utoaji wa ushauri wa kisheria,  hakuna  mianya ya rushwa.
Akasema,Takukuru inaridhishwa sana na taarifa za kwamba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa   Serikali itafanya kazi na kufuatilia kwa karibu michakato ya uandishi wa sheria ndogo ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwamba baadhi yake zinaviashiria vya rushwa , utoaji wa hongo na ukandamizaji.
“Niwasihi pia kwamba,  hata katika Sheria  nyingine na Mikataba mbalimbali,  muendelee kuisaidia serikali kwa kubaini mianya au viashiria vya  rushwa”.
Bw. Mwaisalo alizungumzia pia kwa kina  kuhusu madhara ya rushwa ya ngono na akawataka wanawake na wasichana katika nafasi zao mbalimbali kujiamini kwamba wanaouwezo  mkubwa na haki ya   kupata haki yao ikiwamo ajira pasipo kutoa rushwa ya ngono ambayo ameitaja kuwa ni udhalillishaji wa   hali  ya juu.
“Rushwa ya ngono ni udhalilishaji wa hali ya juu, mwanamke au msichana unauwezo  na  haki ya kuikataa, mjiamini.  Rushwa  ya ngono ni matokeo ya  mmomonyoko  wa maadili na inatakiwa kupingwa kuanzia katika ngazi ya familia zetu. Na viogozi ni muhimu mtambue kwamba uongozi ni dhamana na si vinginevyo”.
 Awali akifungua mafunzo hayo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa. Amesema, kufanyika kwa mafunzo  hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango kazi ambao Ofisi imejiwekea.
Akasisitiza kwamba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Taasisi ya Umma inayowajibu na inawajibika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa.
“Ni kwa sababu  hiyo, tumeandaa mafunzo haya kwa kushirikiana na TAKUKURU ili tuwezeshwe na kukumbushwa kwa kupewa elimu na kufundishwa kuhusu kanuni, taratibu na sheria zinazohusiana na mapambano dhidi ya rushwa”.  Akasema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Na kusisitiza “ Niwaombe watumishi wenzangu tujiepushe na yale ambayo yanaweza kututia matatizoni kwa sababu tu ya kutozingatia kanuni, taratibu na  sheria”amesema Bw. Joseph Mwaisalo na kuongeza. “


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...