Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Klabu ya Soka ya Simba imemsajili Kiungo wa Kimataifa wa Msumbuji, Luis Jose Miquissone ambaye alikuwa akicheza katika Klabu ya UD Songo ya nchini humo, timu iliyoiondoka Simba SC katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Simba SC kupitia Mitandao yake ya Kijamii imetangaza usajili wa Kiungo huyo aliyekuwa Nahodha wa UD Songo lakini haikuweka wazi mkataba wa muda gani.
Usajili wa Jose Miquissone kwa Simba unakuwa wa kwanza katika dirisha hili wakati pia kukiwa na homa ya pambano lao dhidi ya Yanga SC, Januari 4, 2020 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kuelekea pambano hilo, Yanga SC wametangaza kumrudisha nyumbani Kiungo wa Kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo siku za nyuma kabla ya kusajili na Simba SC, Niyonzima tayari amewasili nchini na tayari ameanza mazoezi na wenzake kuelekea pambano lao dhidi ya Simba SC siku ya Jumamosi.
Hata hivyo, Yanga SC tayari imewasajili Mshambuliaji Ditram Nchimbi, Tariq Seif Kiakala na Mshambuliaji raia wa Ivory Coast aliyekuwa anacheza Gor Mahia ya Kenya, Yikpe Gislain Gnamien.
Mtanange kati ya Simba SC na Yanga SC utapigwa kesho Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, pambano litakaloanza majira ya Saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Swali lakujiuliza Je Nyota hao waliosajiliwa kipindi hiki watapangwa katika pambano la kesho ???
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...