Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ameamua kumfukuza kazi Ofisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Daniel Maleki(30) anayetuhumiwa kuchana kitabu kitakatifu cha Quran huku akisisitiza kuwa Serikali anayoingoza haiwezi kuwa na wafanyakazi wapumbavu.

Akizungumza leo Februari 10 mwaka 2020 wakati wa akizindua majengo ya ofisi za Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam , Dk.Magufuli amesema amefurahishwa na hatua ambazo Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) za kumsimamisha kazi mtu huyo na kuongeza kuwa yeye anamfukuza kazi moja kwa moja.

"Juzi nimeona mtu mmoja kule Kilosa nafikiri alikuwa anachana kitabu kitakatifu cha Qurani, nakupongeza Waziri Jafo kwa hatua uliyochukua ya kumsimamisha kazi lakini mimi namfukuza moja kwa moja , ashinde kesi au ashindwe namfukuza kazi, hatuwezi kuwa na wafanyakazi wapumbavu katika Serikali hii.

"Muandikie barua ya kumfuta kazi. Mtu huyo akitoka huko kwa adhabu ambayo ataipata atajua mwenyewe pa kwenda kutafuta maisha,"amesema Rais Magufuli.

Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro lilitangaza kumshikilia Ofisa huyo biashara baada ya kuchana na kuchoma moto kitabu cha Juzuu Amma.Hata hivyo alifikishwa Mahakamani na kukosa dhamana.Wakati akiendelea kusota mahabusu, Waziri wa TAMISEMI Selemen Jafo alitangaza kumsimamisha kazi mtu huyo na leo hii Rais amesema anamfukuza kazi moja kwa moja.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...