Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imetoa ruhusa kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kuwatoza fedha wale wote wanaohitaji takwimu za hali ya hewa kwa ajili ya usanifu miradi mbalimbali ili kufanya kazi za kisanifu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho alipokua akifungua mafunzo yenye lengo la kudhibiti na kusaidia ukusanyawashiriki paato kwa menejimenti ya Mamlaka hiyo ya hewa.
Dk.Chamuriho amesema kuwa wanaosanifu muindombinu ya ujenzi kama vile madaraja wanataka kujua mtiririko na wingi wa maji ili waweze kusanifu madaraja hayo kama yanaweza kuhimili nguvu za asili hivyo kama wanahitaji takwimu hizo TMA ndio sehemu pekee ya kuzipata hivyo ni lazima watozwe fedha.
Amesema Mamlaka ya hewa imekua ikilega katika kukusanya mapato hasa katika huduma ambazo huwa wanazitoa ilihali wao hutumia fedha wakati wa kuandaa takwimu hizo.
" Ni vema sasa mkaanza kuchaji fedha kwenye hizo huduma ambazo mnazitoa. Hiyo itasaidia pia kukuza mapato ya mamlaka ambapo kiasi kitachopatikana kitasaidia katika miradi yetu mingine tunayoifanya.
Wahandisi wengi lazima waje kwenu TMA kabla hawajasanifu majengo yao lakini nyie wala hata hamuwatozi. Kama wao wanachukua takwimu kutokana kwenu na kwenda kujenga majengo makubwa ya kibiashara yatakayowapa fedha kwanini na nyie msiwatoze gharama fulani ili na nyingi muingize pesa?" Amehoji Dk Chamuriho.
Katibu Mkuu pia amesifu utendaji kazi wa TMA na kusema kuwa ubora wa huduma za hali ya hewa umezidi kuongezeka na kuonekana kwa jamii kwa kiwango kikubwa hivyo waongeze bidiii hiyo pia katika ukusanyaji wa mapato yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TMA Dk Agnes Kijazi, amesema mafunzo hayo yanayotolewa kwa Menejimenti ya Mamlaka hiyo yataongeza uwezo na kuwa chachu kwao katika kutoa huduma bora yenye kukidhi haja za wananchi.
Dk Kijazi amesema mafunzo hayo yatahusisha majadiliano kwa washiriki pamoja na mazoezi mbalimbali ya kuwaongezea utimamu huku pia akisema kiwango cha ubora wa TMA umeongezeka ndani ya miaka 10 kufikia asilimia 80 na kuvuka kiwango cha chini kilichowekwa na shirika la hali ya hewa duniani cha asilimia 70.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) Agnes Kijazi akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea ubora Menejimenti ya Mamlaka hiyo. Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Menejiment ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) ambapo mafunzo hayo yanafanyika jijini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo ya kuongeza ubora na utimamu kutoka Menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho wakati wa kufungua mafunzo hayo leo jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...