NAIBU Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu OR-TAMISEMI Gerald Mweli amesema ameridhishwa na kutambua jitihada zinazofanywa na viongozi wa Wilaya ya Chato katika kuwekeza kwenye miundombinu ya Elimu.
Mweli ameyasema hayo wakati alipotembelea Wilaya hiyo na kukutana na Menejimenti, Walimu pamoja na kukagua ujenzi wa shule mbalimbali zilizoboreshwa na zinazoendelea kuboreshwa Wilayani hapo.
Mweli amesema anatambua jitihada kubwa zinazofanywa katika eneo hili la Elimu ikiwa ni pamoja na kuanzisha kiwanda cha matofali ambayo yatatumika katika ujenzi wa madarasa lengo likiwa ni kukuza sekta ya Elimu Wilayani Chato.
‘Naona mmeshafyatua matofali zaidi ya elfu tano na kazi inaendelea hii inanitia moyo, Kazi hii mnayoifanya itasaidia katika kupunguza gharama za ujenzi wa madarasa hapa Chato kushuka kutoka Milioni 20 mpaka Milioni 10 kwa darasa moja kwahiyo kupitia mpango huu mtaweza kujenga madarasa ya kutosha’
Wilaya hii inawatoto wengi ambao wako shuleni na wengine wanakaribia kuanza shule hii inapelekea mahitaji makubwa ya vyumba vya madarasa ili watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaende na wapatiwe elimu bora," Amesema Mweli.
Katika kikao chake na Menejiment ya Halmashauri ya Wilaya Chato Mweli alisisitiza ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo kwa mwaka huu wa Fedha halmashauri hiyo inatakiwa kukusanya Bil 2.9 pia alipokea taarifa ya utoaji wa mikopo ya wanawake, vijana na walemavu.
Aidha wakati akizungumza na Walimu, Mweli alitolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyoibuliwa na kutolea ufafanuzi katika kupanda madaraja kuwa kigezo si muda tu bali ni utendaji kazi, namna ulivyopimwa kwenye Opras pamoja mahitaji ya nafasi hiyo kwa wakati husika.
" Kupanda madaraja sio kufikisha muda tu kuna sifa nyingi za ziada zinazoangaliwa kama hujazifikia zote huwezi kupanda hata kama muda wako umefika hivyo tunatakiwa kujituma na kuleta matokeo katika maeneo yetu ya kazi wakati wote’ alisisitiza Mweli.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliud Mwaiteleke amesema halmashauri hiyo imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha inakuanya mapato ipasavyo na fedha hizo zinaenda kutekeleza miradi ya maendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Pia aliishukuru Serikali kwa kuwapatia vitendea kazi kama vile Mashine za kukusanyia mapato (POS) 43 ambazo kwa kiasi kikubwa zimedhibiti upotevu wa mapato.

Watumishi mbalimbali wa Wilaya ya Chato wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anaeshughulikia elimu, Gerald Mweli alipofanya ziara ya kikosi wilayani hapo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anaeshughulikia elimu, Gerald Mweli akizungumza na viongozi na watumishi wa Wilaya ya Chato alipofanya ziara ya kukagua miundombinu kwenye sekta ya elimu.
Naibu Katibu Tamisemi anaeshughulikia elimu, Gerald Mweli akikagua kiwanda kidogo cha kufyatulia matofali ambayo yanatumika kujengea madarasa kwenye shule za Wilaya hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...