Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akisalimiana kwa
mtindo wa kugonganisha miguu na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Farkwa
wilayani Chemba alipofika katika kijiji hicho kuwasha umeme na kukagua
maendeleo ya usambazaji wa umeme katika wilaya hiyo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Chemba, Saimon Odunga( katikati)wakiteta jambo wakati Dkt. Kalemani
alipofika katika wilaya hiyo kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akitoa maelekezo kwa
Mameneja wa TANESCO na REA kusimamia uondoaji wa nguzo za umeme
zilizolazwa chini katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Chemba.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akikagua baadhi ya
nguzo za umeme zilizolazwa chini katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya
Chemba.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Farkwa wakimsikiliza Waziri wa Nishati,
Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) alipofika katika wilaya hiyo
kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wazee wa kijiji cha Farkwa waliopewa vifaa vya
umeme tayari( UMETA), baada ya waziri kuwasha umeme katika kijiji hicho
Wilaya ya Chemba.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wakazi wa kijiji cha Babayu wilayani Chemba, baada ya waziri huyo kukagua maendeleo ya usambazaji umeme katika kijiji hicho.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akipokea zawadi ya mbuzi
kutoka kwa mmoja wa wazee wa Kijiji cha Babayu wilayani Chemba, baada
ya waziri huyo kukagua maendeleo ya usambazaji umeme katika kijiji
hicho.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wakazi
wa kijiji cha Makorongo wilayani Chemba, baada ya wanakijiji hao
kusimamisha msafara wa waziri huyo ili kutaka kujua lini wanaletewa
umeme wakati akikagua maendeleo ya usambazaji umeme katika wilaya hiyo.
Na Zuena Msuya Dodoma,
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa onyo na kupiga marufuku wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini nchi nzima, kulaza nguzo za umeme chini kwa muda mrefu,badala yake ndani ya siku tatu nguzo hizo ziwe zimefikishwa eneo la mradi na kusimikwa.
Pia alitoa muda wa siku tatu kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa REA mkoani Dodoma kuondoa nguzo zote ambazo zimelazwa chini katika Mkoa huo na kuzisimika katika maeneo husika, kinyume cha hapo mhandisi na mkandarasi watachukuliwa hatua.
Dkt. Kalemani alitoa onyo hilo, Machi 4, 2020, wakati wa kuwasha umeme katika kijiji cha Farkwa kilichopo wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Alisema kumekuwa na tabia ya wakandarasi kuacha nguzo zikiwa chini kwa muda mrefu bila kusimikwa jambo ambalo limesababisha baadhi ya nguzo kuharibika na fedha za serikali kupotea.
Aidha, Dkt. Kalemani aliwataka Wakurugenzi wa Tanesco na Mkurugenzi wa REA kuhakikisha wanasimamia maagizo hayo kwa ukaribu na umakini.
“Hili ni onyo la mwisho, nimepita barabarani nimekuta nguzo zimelala, sasa Meneja wa TANESCO Kanda na Mikoa simamieni maelekezo haya nguzo zote zilizolazwa chini kwenye mikoa nchi mzima ziondolewe na zikajengwe”, alisema Dkt. Kalemani.
“Nasema siku tatu kutoka leo, Machi 4, 2020, nguzo zilizolazwa chini mkoani Dodoma ziondolewe, tofauti na hivyo mhandisi achia ngazi, mkandarasi utaandikiwa barua ya kufuta mkataba wako, nakueleza mapema tena hadharani! meneja lisimamie hili”, alisisitiza Dkt.Kalemani.
Alisema serikali imetoa Shilingi bilioni 40.2 kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini.
Dkt. Kalemani alisema kuwa Serikali inavitu vingi vya kuwahudumia wananchi kama sekta ya maji, afya, barabara na elimu lakini bado imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kuhakikisha vijiji vyote vinapatiwa umeme.
Alisema pamoja na juhudi za serikali za kupeleka umeme maeneo mengi, lakini bado kuna changamoto kwa baadhi ya maeneo ambayo hayajafikiwa na kuwa serikali inafanya kila liwezekanalo kuiangaza Tanzania yote.
“Na hili ni onyo kwa wakandarasi wote nchi nzima ni marufuku kuanzia sasa nguzo kulazwa chini kwa muda mrefu, zikifika ndani ya siku tatu zikasimikwe na zikajengwe ili wananchi wakapate umeme.”
Akizungumzia uwashaji wa umeme katika kijiji cha Farkwa, Dkt. Kalemani alisema uwashwaji wa umeme katika kijiji hicho unaifanya idadi ya vijiji vya Wilaya ya Chemba vilivyofikiwa nishati ya umeme kufikia 85 kati ya vijiji 114, na kuwahidi wananchi wa eneo hilo kuwa vijiji vyote vilivyosalia pia vitafikiwa na umeme ndani ya muda uliopangwa.
Aidha, Dkt.Kalemani aliwaagiza Mameneja wa REA na TANESCO kuhakikisha vijiji vilivyobaki katika kata ya Farkwa kufikishiwa nishati hiyo ndani ya miezi miwili ijayo na kumuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga kusimamia hilo.
Pia alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kutumia umeme huo kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi ikiwamo uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo na kuwa hiyo itakuwa ni kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.
“Haiwezekani serikali ikatoa fedha ya kuwafikishia wananchi umeme tena kwa gharama nafuu, halafu wewe mwananchi usiutumie, tutapita kila kaya kukagua na tukikuta hujaweka umeme tutapiga mnada na kuuza kuku au mbuzi na kukuwekea umeme kwa lazima,hivyo hakikisheni mnajiunganishia nishati hiyo”, alisema Dkt. Kalemani
Pia aliwasihi wananchi wa Farkwa na maeneo mengine kuhakikisha wanatunza miundombinu ya umeme ili iweze kuwasaidia wananchi.
Naye Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia pamoja na kuipongeza serikali kwa kazi ya kuwafikishia wananchi nishati hiyo aliomba maeneo ambayo bado hajafikiwa yafikiwe ili wananchi waweze kujiletea maendeleo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kuunganishwa umeme kwa Shilingi 27,000 kupata huduma hiyo wakati mradi unaendelea.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...