Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akisema jambo kwa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya (hawapo
pichani) wakati wa ziara katika Gereza Kuu la Arusha.
ACP Dkt. Richard Mwankina akisoma taarifa ya Jeshi la Magereza kwa niaba
ya Kamishna Generali wa Magereza Suleiman Mzee (hayupo pichani) kwa
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya
Kulevya.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Leonard Subi
akisema jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na
Madawa ya Kulevya na viongozi waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini
(hawapo pichani)
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya
Kulevya wakisalimiana na maafisa wa Gereza kuu la Arusha walipofanya
ziara gerezani hapo kuzungumza na wafungwa na mahabusu.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya
Kulevya pamoja na wataala kwenye kikao cha pamoja wakijadiliana masuala
ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya gerezani katika kikao kilichoongzowa na
Mwenyekiti Mhe, Oscar Mukasa
Na Englibert Kayombo WAMJW -Arusha
Juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi zimeliwezesha Jeshi la Magereza kuboresha huduma za matibabu na upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (VVU) hivyo kufikia malengo ya milenia (90-90-90)
Hayo yamesemwa na Uongozi wa Jeshi la Magereza wakati wa kikao na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanahusika na masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya.
Akisoma taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU na upatikanaji wa tiba kwa magonjwa nyemelezi kwa niaba ya Kamishna Jenereali wa Magereza Bw. Suleiman Mzee, ACP. Dkt. Richard Mwankina amesema “huduma za Afya gerezani zimeboreshwa kwa kiwango cha juu na imetusaidia kuweza kuboresha matibabu na upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya VVU kwa wagonjwa”
ACP.Dkt. Mwankina amesema kuwa kutokana na juhudi za Serikali za kupambana na VVU kumekuwa na ongezeko la wafungwa na mahabusu kujitokeza kwa hiari kupima afya zao hivyo kufikia lengo la kwanza (1st 90) ambapo baada ya kuwagundua wagonjwa wa VVU waliweza kuwaanzishia dozi na kuwa na ufuasi mzuri wa dawa (2nd 90) Wagonjwa hao wamekuwa na matokeo mazuri ya ufubazi wa VVU (3rd 90) hivyo kufikia malengo ya milenia (90-90-90)
ACP. Mwankina amesema kuwa wamefanikiwa kufikia malengo hayo ya milenia kutokana na mikakati madhubuti ya kuhakikisha wanatoa na kusimamia huduma za afya kwa wafungwa, mahabusu pamoja na wataalam na familia zao.
“Kabla ya Mwaka 2007 watumishi wa Jeshi la Magereza na familia zao, wafungwa pamoja na mahabusu walikuwa wanapata huduma za afya katika vituo vya nje” amesema ACP. Dkt. Mwankina
ACP. Dkt. Mwankina amesema kuwa kuanzia mwaka 2007 huduma za afya zilianza kutolewa ndani ya Jeshi la Magereza na walianza kujenga vituo hivyo ambavyo mpaka kufikia mwaka 2020 idadi ya vituo hivyo vimefika 30.
Amefafanua kuwa kupitia vituo hivyo wameweza kufanya upimaji wa hiari kwa wafungwa na mahabusu katika nyakati tofauti ambapo walifanikiwa kuwabaini wagonjwa wa VVU na kuwaanzishia dozi ya kufubaza makali ya VVU.
“Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2019, jumla ya wafungwa na mahabusu 1372 katika Gereza Kuu la Arusha walijitokeza kwa hiari kupima afya zao na tuliwabaini wa 34 kuwa na VVU, kati yao 31 ni wanaume na watatu ni wanawake” amesema ACP. Dkt. Mwankina
Amesema kuwa wameweza kufikia mafanikio haya kutokana na elimu ambayo wafungwa na mahabusu wamekuwa wakiipata ambapo walijitokeza na kupima afya zao pamoja na kuimarisha ushirikiano mzuri baina yao na vituo vya kutolea huduma za afya nje ya magereza ili kuweza kupata huduma za rufaa za matibabu pindi ambapo huduma za vipimo na tiba zaidi zinapokosekana ndani ya gereza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya. Dkt. Leonard Subi amesema kuwa Serikali imekuwa ikitoa mafunzo ya masuala ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Ukimwi na TB katika magereza ambapo kwa mwaka 2019 jumla ya magereza 17 yalinufaika na mafunzo hayo.
“Mwaka jana tumeweza kutoa elimu ya magonjwa ya kuambukiza kwa magereza 17 nchini, ambapo tulitoa mafunzo kwa maafisa magereza 209 na watumishi wengine 1378” amesema Dkt. Subi na kuendelea kusema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wataalam, wafungwa na mahabusu kutambua dalili na athari zitokanazo na magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Ukimwi na Kifua Kikuu”
Dkt. Subi amesema kuwa pamoja na mafunzo hayo waliendeshazoezi la upimaji wa hiari kwa wafungwa na mahabusu ambapo jumla ya wafungwa 5005 na mahabusu 6795 walipimwa afya zao.
“Katika upimaji huo tulibaini uwepo wa waginjwa 42 wenye ugonjwa wa kifua kikuu na tuliweza kuwaanzishia matibabu mara moja” amesema Dkt. Subi
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Suleiman Mzee amesema kuwa Jeshi la magereza ni moja ya wahanga wa ugonjwa wa VVU na hawapo nyuma katika kupambana na ugonjwa huo kwa wafungwa, mahabusu, watumishi na familia zao.
Kamishna Mzee amesema kuwa Jeshi la magereza linatoa huduma za uchunguzi wa afya, tiba, ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya ukimwi pamoja na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
“Jeshi la Magereza lina jukumu la kuhakikisha wafungwa na mahabusu wanapata huduma bora za afya kama ilivyo kwenye jamii nyingine” amesema Kamishna Suleiman Mzee.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...