
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watoto sita raia wa Ethiopia akiwemo mwenye umri wa miaka mitano baada ya kukuta wamehifadhiwa kwenye nyumba ya mtu binafsi eneo la Ngureso katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Akizungumzia tukio hilo leo Kamanda wa Polisi omkoani hapa Jonathan Shanna amesema kuwa watoto hao wenye umri wa miaka mitano hadi 12 waligundulika Februari 20 mwaka huu kuhifadhiwa nyumbani kwa Amina Ally na Mohammed Mahamudu mkazi wa Ngusero jijini Arusha.
Kamanda Shanna amefafanua kuwa Polisi walipata taarifa kuwa nyumbani kwa Amina kuna watoto wamefichwa na kwamba watoto hao walikuwa hawajui lugha yoyote za hapa nchini ndipo polisi walipovamia katika nyumba hiyo na kufanikisha kuwakuta watoto hao sita akiwemo mwenye umri wa miaka mitano
Amewataja watoto hao kuwa ni ,Rukia Tajibu Ismail(12),Zainabu Tayibu(11)Kuruthunu Tayibu(10)Yimaji Tayibu(9)Arafat Tayibu (5) pamoja na Umayi Tayibu wote wakiwa RAIA wa Ethiophia.
Aidha Kamanda Shana ameongeza mara baada ya kuwahoji watoto hao wamedai kuwa walitoroshwa kutoka nyumbani kwa mama yao nchini Ethiopia ili wapelekwe Afrika Kusini kwa baba yao kupitia Nairobi nchini Kenya na wameingia nchini kupitia mpaka wa Namanga.
Aidha Kamanda Shana amesema wakati wanaendelea kuwahoji watoto hao alijitokeza Ateyibo Isumail Yusuf(45) kutoka nchini Afrika Kusini akidai kwamba yeye ni baba wa watoto hao.
Hata hivyo Polisi walimtilia shaka na kuamua kumshikilia katika kituo cha Polisi baada ya kubaini hana kibali halisi cha kuingia nchini .
Kamanda Shana amedai kuwa Polisi wamechukua vipimo vya vina saba kwa watoto hao na mtu huyo anayedai ni baba wa watoto hao ili kujiridhisha kama kweli ni baba wa watoto hao.
Polisi bado inawasiwasi kuwa huenda watoto hao walikuwa wanasafirishwa kwa ajili ya kufanyiwa biashara ya haramu ya binadamu kupitia nchi ya Tanzania.
Kamanda Shana amesema kwa sasa jeshi hilo linawasiliana na askari wa kimataifa (Enter pool) kwa ajili ya kuwarejesha watoto hao nchini kwao Ethiopia na kwamba Eteyibo Isumail anayedai ni baba wa watoto hao atafikishwa mahakamani kwa kosa la kuingia nchini bila kufuata sheria.
Watoto hao ambao walikamatwa tangu Februari 20 mwaka huu wanafikisha siku 19 wakiwa bado wanasota mahabusu ya jeshi la polisi jijini Arusha wakisubiri uchunguzi wa jeshi la polisi .
Hata hivyo watetezi wa haki za binadamu,bi Hasna Ally mkazi was jijini Arusha amelitaka jeshi hilo kuangalia njia sahihi ya kuwasaidia watoto hao kuwa Huru kuliko kuendelea kuwashikilia kutokana na umri wao kuwa mdogo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...