Na Leandra Gabriel na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
PROGRAMU ya  Taifa ya mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wa elimu ya juu (Intership Training Program) imezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hafla iliyoenda sambamba na ufunguzi wa mkutano na mawaziri wa sekta ya kazi na ajira na wadau wa utatu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC.)

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Samia amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwaandaa wahitimu kuweza kupata uzoefu wa kazi na ujuzi wa kuajiriwa na kujiajiri, na kueleza kuwa Serikali ya Tanzania umeweka jitihada katika hilo na hadi sasa  wahitimu 5967 wamehitimu mafunzo hayo huku wahitimu 1827 wakiwa wameajiriwa hasa katika sekta binafsi.

Aidha amezishauri  nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC kuanzisha utaratibu huo ili ulete manufaa ya vijana ndani ya Jumuiya hiyo.

"Mara nyingi vijana wasomi wanapomaliza masomo yao hukosa ajira kutokana na kigezo cha kukosa uzoefu wa kazi suala ambalo Serikali tumeliona na tumelitafutia ufumbuzi" Amesema Samia.

Kuhusiana na mkutano wa Mawaziri na sekta ya kazi na ajira na wadau wa utatu wa SADC uliobeba kauli mbiu ya "kukuza Soko la Ajira na Mahusiano Mazuri Sehemu za Kazi kwa Maendeleo Endelevu"  Samia amesema kuwa yatakayojadiliwa katika mkutano huo tija katika katika sekta ya kazi na ajira pamoja na kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo na ufanikisha utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) hasa lile linaalohimiza fursa za ajira zenye staha.

Pia amewahimiza wadau wa utatu kuweka mazingira ya kisera na miongozo itakayowezesha uhamasishaji wa Sheria na kanuni katika nchi wanachama kwa kuweka misingi ya haki na usawa katika kupata fursa za ajira na kuimarisha mahusiano mema Kati ya waajiri na wafanyakazi.

Kwa upande wake katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt. Stergomena Tax amesema kuwa ukuzaji wa viwanda ndani ya Jumuiya utachangua sana katika kutengeneza ajira pamoja na kukuza soko.

Amesema kuwa Serikali ya Tanzania imekua mfano katika kukuza na kutengeneza ajira mpya kwa kuanzisha programu ya vitendo mahala pa kazi jambo ambalo lina faida kubwa ndani ya Jumuiya na kuzishauri nchi wanachama kujifunza utaratibu huo ambao una tija.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri wa sekta ya kazi na ajira kutoka nchi wanachama 14 isipokuwa Mauritius and Commoro.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya kazi, Ajira na Wadau wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo Machi 05,2020.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizindua Mpango maalum wa Mafunzo kwa Vitendo katika sehemu ya kazi kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya kazi, Ajira na Wadau wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo March 05,2020.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akionesha Mpango maalum wa Mafunzo kwa Vitendo katika sehemu ya kazi mara baada ya kuzindua mpango huo katika Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya kazi, Ajira na Wadau wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo Machi 05,2020.kushoto Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama kulia katibu Mtendaji wa jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Dr. Stergomena Tax na Waziri wa Kazi Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mouldine Castico.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Tuzo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela kwa kutambua mchango wake wa Udhamini kwa Vijana katika Mpango Maalum wa Mafunzo Sehemu ya kazi kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya kazi, Ajira na Wadau wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo Machi 05,2020.
Picha ya Pamoja ya viongozi mbalimbali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Cheti kwa Agatha Masola kati ya Vijana 20 wanaoendelea na Mpango Maalum wa Mafunzo Sehemu ya kazi wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya kazi, Ajira na Wadau wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo March 04,2020.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...